Maulama wa Kisuni katika mji wa Mosul Iraq,
wametangaza vita vya jihadi dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh linaloungwa
mkono na Marekani.
Maulamaa na mamufti |
Maulamaa na mamufti wa mji huo wametangaza hatua
hiyo katika kongamano lililofanyika mjini Erbil, Kurdistan ambapo pamoja na
mambo mengine wametangaza kuwa, kundi hilo lisilofuata mafundisho ya Kiislamu,
linawatumia raia wa mji wa Mosul kama ngao na kwamba wananchi wanatakiwa
kupambana na matakfiri hao.
Wanavyuoni hao wamefafanua kuwa, ni wadhifa wa
maulama wa kidini kuisafisha sura ya Uislamu baada ya kuchafuliwa na kundi hilo
hasa kwa kuzingatia kuwa, baadhi ya maulama huko Mosul wanalazimika kutoa fatwa
zinazoendana na matakwa ya kundi hilo wakiwa chini ya mashinikizo na vitisho.
Katika upande mwingine jeshi la Iraq limekama chombo
cha kijasusi cha kielektroniki cha utawala haramu wa Kizayuni wa Israel
kilichokuwa kikitumiwa na kundi hilo la Daesh.
Kwa mujibu wa jeshi hilo, chombo hicho kimenaswa
katika operesheni za kuukomboa mji wa Tikrit, makao makuu ya mkoa wa Salahuddin
ambao umekaribia kukombolewa kikamilifu kutoka kwa magaidi hao na kwamba
kimenaswa katika uwanja wa ndege wa ad Daur, mashariki mwa mji huo.
No comments:
Post a Comment