Kwa mara nyingine Waislamu nchini Nigeria wamefanya
maandamano ya amani wakitaka kuachiliwa huru Sheikh Ibrahim Yaqoub El
Zakzaky, kiongozi wa harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo.
Mamia ya Waislamu wamemiminika mabarabarani katika jimbo ka
Kano, kaskazini mwa nchi hiyo na kutaka kuachiliwa huru haraka
iwezekanavyo kiongozi huyo wa harakati ya Kiislamu nchini Nigeria.
Hii
ni katika hali ambayo maelfu ya wananchi mjini Abuja, mji mkuu wa
Nigeria walifanya maandamano makubwa hapo siku ya Jumatano katika
kulalamikia hatua ya serikali ya Rais Muhammadu Buhari ya kuzidisha
mashinikizo dhidi ya Waislamu wa taifa hilo na kutaka kuachiliwa huru
Sheikh Ibrahim El Zakzaky anayeendelea kuwekwa kizuizini.Ni miezi minane sasa imepita tangu kiongozi huyo wa Kiislamu na mke
wake Zeenat walipotiwa mbaroni na jeshi la Nigeria. Hii ni katika hali
ambayo hali ya kiafya ya kiongozi huyo imetajwa kuwa mbaya mno, hata
hivyo viongozi wa nchi hiyo hawako tayari kusikiliza malalamiko ya
wananchi ya kumuachilia huru.Katika uvamizi wa jeshi la Nigeria kwenye makazi ya Sheikh huyo mjini
Zariya katika jimbo la Kaduna kaskazini mwa nchi hiyo na pia dhidi ya
Husseiniyyah ya Waislamu wa Kishia hapo tarehe 14 Disemba mwaka jana
2015, karibu Waislamu 1000 waliuawa. Kadhalika jeshi hilo lilimjeruhi
kwa risasi kadhaa Sheikh Ibrahim Yaqoub El Zakzaky na mke wake na kisha
kuwatia mbaroni na kuendelea kuwashikilia hadi sasa.chanzo.parstoday