Na: Twalha Ndiholeye
Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Mhe. Mussa
Farhang amewataka Wananchi wa Tanzania hususani Wasomi, Wanachuo na
Wananasiasa kutokuruhusu uingiliaji wa
Siasa za Madola ya Kigeni katika siasa ya ndani ya nchi na kuwataka wasiwe
tegemezi ili kuenzi Uhuru na Amani uliopo.
“Wananchi wa Tanzania, Jamii ya Wasomi, Wanachuo na Wanasiasa
wasiruhusu kabisa ule uingiliaji wa siasa wa Madola ya Kigeni katika siasa za
ndani,tusiwe tegemezi kwani Uhuru wetu hautakuwa na faida yoyote, dhamani
yoyote na nguvu yoyote” alisema Balozi Farhang.
Balozi wa Iran Mhe. Farhang alisema hayo jana katika Semina
ya kuelekea maadhimisho ya Miaka 40 ya Serikali ya Mapinduzi ya Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran, iliyofanyika katika Chuo cha Diplomasia, Kurasini jijini Dar
es salaam.
Aidha Balozi Mhe.Farhang amewataka Watanzania kuenzi Fikra za
Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na Imam Khomein katika kuheshimu Sheria ambapo
ndio chanzo cha utekelezaji wa maendeleo na udumishaji wa Amani na maelewano
uliokusudiwa na waasisi wa nchi.
“Tufate zile fikra za Viongozi wetu waasisi wa Mataifa yetu
Baba wa Taifa Mwl. Nyerere na Imam Khomein, lakini wenye Umuhimu sana kwa
wananchi wa Tanzania kufuata na kuenzi fikra za Mwl.Nyerere, Ufuataji wa Sheria
ni kitu ambacho lazima iheshimiwe kwani ndio chanzo cha maendeleo, Tusaidie
Tanzania na Irani ziweze kuendelea kufuata mfumo wa Sheria.”.aliongeza Balozi.
Mapinduzi ya
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yalifanyika mwaka wa 1979, yakiongozwa na Kiongozi
wa Kiongozi wa Kidini ajulikanae kwa jina la Imam Khomein ambae alifaniliwa
kumuondoa Mfalme Shaah amabe alikuwa Kiongozi wa nchi ya Iran kipindi hicho.