Thursday, May 24, 2018

DAWA ZAVUSHWA KUPITIA MTO WENYE MAMBA MKOANI RUVUMA

WANANCHI wanaoishi katika Vijiji vya Mkenda na Mitomoni vilivyopo kandokando ya mto Ruvuma wilayani Nyasa mkoani Ruvuma wamesema changamoto kubwa waliyonayo ni 
mazingira magumu ya miundo mbinu ambayo inasababisha ugumu wa ufikishaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kutoka  Bohari ya Dawa (MSD).

Wakazi hao wamesema kuwa, mazingira ya kufikisha dawa kwenye vijiji hivyo hutegemea zaidi usafiri wa kuvuka mto Ruvuma ambapo hulazimika kutumia boti,ambapo hata hivyo maisha yao yanakuwa na mashaka ndani ya mtumbwi hiyo ambayo iko wazi kutokana na mto huo kuwa na mamba wengi.

"Changamoto yetu kubwa ni usafishaji wa dawa kuja hapa kijijini kutokana na kutegemea zaidi mto huu ambao una mamba wengi, hata mwaka huu mwanzoni mtumbwi huu mnaouona ulipinduka na watu  wakiwapo wauza mitumba waliuawa na mamba; lakini tunashukuru  Bohari ya Dawa (MSD) kwani wao wanaweza kutuletea dawa  kwa wakati" alisema Mwenyekiti wa kamati ya Afya wa kijiji cha Mitomoni Omar Hassan.

Alisema ili kuondoa changamoto hiyo, wanaiomba serikali kuhakikisha inaboresha miundombinu ya barabara, ili dawa hizo zisafirishwe kwa njia ya barabara badala ya kutegemea mto huo. 

Alisema yeye na kamati yake wamekuwa wakipokea dawa mara nne kwa mwaka kutoka MSD na kuzihakiki kwa ajili ya matumizi.

"Pamoja na changamoto ya miundombinu lakini tumekuwa tukihakikisha dawa zinazoletwa na MSD zinafika kituoni na kutumika ipasavyo,"alisema.

Alisema kutoka Songea mjini hadi Kijiji cha Mitomoni, Songea vijijini, katika kituo hicho cha afya ni km 135 na MSD imekuwa ikihakikisha dawa hizo zinafika.

Alisema changamoto zinakuwa kubwa zaidi kipindi cha mvua kwa kuwa miundombinu ya barabara hadi kufika kivukoni ni tatizo na kuna wakati dawa zinafika usiku na zinatakiwa kuvushwa usiku huo huo.

Hassan alisema changamoto hiyo ya mamba katika mto huo anaijua vizuri kwani mtoto wake Sanifu Omar (27), alipoteza maisha kwa kuliwa na mamba wakati alipokuwa akisafirisha abiria kwa kutumia mtumbwi.

Mkazi wa Kijiji cha Mitomoni Khadija Salum alisema wamekuwa wakipata dawa zote muhimu katika kituoni hicho ikiwemo za mama mjamzito na mtoto bila ya ubaguzi na kwa wakati.

"Mimi nina watoto watano kuanzia ujauzito wa kwanza sijawahi kukosa dawa hapa pamoja na ugumu wa miundombinu lakini dawa zinafika hivyo serikali ione haja ya kuboresha barabara zetu," alisema.

Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mitomoni, Ivo Hekela, alisema kijiji hicho kinahudumia agonjwa 12,000 kutoka vijiji vitano ambavyo ni Mitomoni, Mipotopoto,Konganywita,Mkenda,Uhuru na Mozambique. 

Meneja wa MSD Kanda ya Iringa, John Sipendi, alisema wamekuwa katika changamoto ya kufikia vituo hivyo vya pembezoni ikiwa ni pamoja na kutumia muda mrefu kufikisha dawa na wakati wa mvua kukwama kwa magari njiani na gharama za usafirishaji kuogezeka.

Madereva wa MSD Kanda ya Iringa wamesema wamekuwa wakishindwa kushusha dawa wakati wa mvua za masika kutokana na mto huo kujaa maji hivyo hulazimika kulala kijijini hapo kwa siku mbili hadi tatu.

Tanzania yaombwa kuisaidia Palestina

Kamati ya Mshikamano wa Tanzania na Palestina imeitaka Tanzania kuendelea kushawishi Umoja wa Mataifa kuleta mapatano kati ya Paletina na Israel ili Wapalestina waweze kuwa na Amani katika nchi yao kama ilivyo kwa Watanzania.

Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Ndugu Abdullah Othman wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Juzi jijini Dar es salaam na kusema kuwa tunapozindua ubalozi huko Tel Aviv nivizuri tukakumbuka majanga yanayowapata wenzetu Wapalestina wanaoendelea kukandamizwa na Tukumbuke msimamo aliokuwanao Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere ambae mnamo 1984.

Othmani alisema kuwa kwa Tanzania kufungua Ubalozi wake huko Israel mjini Tel Aviv na kuikaribisha Israel nayo ifungue ubalozi wake nchini Tanzania hakuna pingamizi na hilo bali tunahofia Misimamo iliyosifika nayo Tanzania Kimataifa kudhoofika.

Tunaambiwa yote haya yanatokana na sera yetu mpya ya Diplomasia ya Kiuchumi inayolenga mahusiano yenye maslahi yakiuchumi na nchi yoyo teduniani. Hatuna pingamizi nahilo ila tunatahadharisha isitupeleke kuja kuregeza misimamo yetu madhubuti iliotupaheshima katika anga za kimataifa na misimamo ilioasisiwa na Baba wa Taifa,nayo nikupinga Ukandamizwaji,Uonevu na Ukoloni mambo leo” alisema Othman.
[​IMG]
Pia Othmani aliitaka Serikali kutafakari kwa kina aina gani ya Mahusiano inayojenga kati ya Tanzania na Palestina kwa hatua yake ya kufungua Ubalozi Israel Mjini Tel Aviv na kuikaribisha Israel nchini nayo ifungue Ubalozi wake kwa mlango wa sera mpaya ya Kiuchumi.

Je leo hii katika kipindi hiki tunafungua ubalozi kwa sera mpya ya Kiuchumi na  watajisikiaje ? haliyakuwa  Israel ambayo imewatia gerezani Wapalestina zaidi ya 6,000, wakiwemo watoto 304 na wanawake 63. Hawa ni wafungwa wa kisiasa ambao wamefungwa chini ya sharia yakijeshi. Idadi yao inazidi kuongezeka kila siku.
 Image may contain: 3 people, people smiling
Siku moja baada ya Tanzania  kuzindua Ubalozi wake Israel, Wapalestina  zaidi ya 50 wameuwawa wakiandamana wakiwemo watoto na wanahabari wawili dhidi ya hatua ya Marekani kufungua ubalozi Jerusalem, Zaidi ya Wapaletina 5,500 wamejeruhiwa. Sikumoja tu!