Kamati ya Mshikamano wa
Tanzania na Palestina imeitaka Tanzania kuendelea kushawishi Umoja wa Mataifa
kuleta mapatano kati ya Paletina na Israel ili Wapalestina waweze kuwa na Amani
katika nchi yao kama ilivyo kwa Watanzania.
Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Ndugu Abdullah
Othman wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Juzi jijini Dar es salaam na
kusema kuwa tunapozindua ubalozi huko Tel Aviv nivizuri tukakumbuka majanga yanayowapata
wenzetu Wapalestina wanaoendelea kukandamizwa na Tukumbuke msimamo aliokuwanao Baba
wa Taifa, Mwalimu Nyerere ambae mnamo 1984.
Othmani alisema kuwa kwa
Tanzania kufungua Ubalozi wake huko Israel mjini Tel Aviv na kuikaribisha Israel
nayo ifungue ubalozi wake nchini Tanzania hakuna pingamizi na hilo bali
tunahofia Misimamo iliyosifika nayo Tanzania Kimataifa kudhoofika.
“Tunaambiwa yote haya
yanatokana na sera yetu mpya ya Diplomasia ya Kiuchumi inayolenga mahusiano
yenye maslahi yakiuchumi na nchi yoyo teduniani. Hatuna pingamizi nahilo ila tunatahadharisha
isitupeleke kuja kuregeza misimamo yetu madhubuti iliotupaheshima katika anga za
kimataifa na misimamo ilioasisiwa na Baba wa Taifa,nayo nikupinga Ukandamizwaji,Uonevu
na Ukoloni mambo leo” alisema Othman.
Pia
Othmani aliitaka Serikali kutafakari kwa kina aina gani ya Mahusiano inayojenga
kati ya Tanzania na Palestina kwa hatua yake ya kufungua Ubalozi Israel Mjini
Tel Aviv na kuikaribisha Israel nchini nayo ifungue Ubalozi wake kwa mlango wa
sera mpaya ya Kiuchumi.
“Je
leo hii katika kipindi hiki tunafungua ubalozi kwa sera mpya ya Kiuchumi na watajisikiaje ? haliyakuwa Israel ambayo imewatia gerezani Wapalestina
zaidi ya 6,000, wakiwemo watoto 304 na wanawake 63. Hawa ni wafungwa wa kisiasa
ambao wamefungwa chini ya sharia yakijeshi. Idadi yao inazidi kuongezeka kila siku.
Siku moja baada ya Tanzania kuzindua Ubalozi wake Israel, Wapalestina zaidi ya 50 wameuwawa wakiandamana wakiwemo watoto
na wanahabari wawili dhidi ya hatua ya Marekani kufungua ubalozi Jerusalem, Zaidi
ya Wapaletina 5,500 wamejeruhiwa. Sikumoja tu!
No comments:
Post a Comment