Monday, May 21, 2018

Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania yaftari na Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es salaam.

Kiongozi Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala akiongea katika hafla ya futari ya pamoja na Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es salaam, Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam.
Kiongozi Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala Amewataka Watanzania, Waislamu na Wakritso kuwa na Umoja wa dini zote kwa kurudi katika mafundisho ya Dini zao Quran na Injiri.

Sheikh Jalala amesema hayo jana katika hafla ya Futari ya Maoja na Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es salaama, iliyoandaliwa na Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam na kuwasisitiza Watanzania, Waislamu na Wakristo kudumisha amani, maelewano na masikilizano kwa kuzilia Nafsi zao kwa kumtambua Mwenyezi Mungu vizuri pamoja na Vitabu vyao.

“Katika tunu tunaoililia leo katika nchi yetu ya Tanzania nchi ya watu ambao ni wamaoja, wamekuwa wanaishi pamoja bila kubaguana hata siku moja, wala hawajuani kwa makabila yao, Umoja wa Dini zote ziliopo nchini Tanzania na dini kubwa tulizonazo ni Uislamu na Ukristo, naamini ya kwamba Waislamu na Wakristo wanaweza kuwa kitu kimoja watakaporudi kwenye Vitabu vyao Quran na Injiri vinasemaje” Alisema Sheikh Jalala

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Issa Rwechungura akiongea katika hafla ya futari ya pamoja na Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es salaam, Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam.
Nae Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Issa Rwechungura amesema baadhi ya Wafuasi wa dini ya Kiislamu wamekuwa hawafuati muongozo wa dini ya Kiislamu na hatimae kuwa chanzo cha mifarkano katika Jamii inayowazunguka.

“Tunalazimika kufuata Muongozo wa Dini ya Kiislamu baada ya kuwa tumesilimu, tatizo ndugu zangu ni kwamba baadhi yetu katika waislamu hatuambatani na muongozo wa Dini ya Kiislamu na matokeo yake inatokea Mifarakano kati yetu au kati yetu na wasiokuwa Waislamu, kinyume kabisa na mafunzo ya Mtume Muhammad (s.a.w.w)” alisema Sheikh Rwechungura.

Sheikh Rwechungura amesema kuwa swala la makundi katika jamii yetu ni jambo ambalo lipo na haliepukiki, bali wajibu wetu ndani ya jamii  hususani ya Kitanzania ni kutafuta muafaka wa kuishi kwa amani ili amani hiyo ituwezeshe kutekeleza majukumu yetu ya kirofo na ya Kijamii.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Al Bukhar Foundation Sheikh Khalifa Khamisi akiongea katika hafla ya futari ya pamoja na Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es salaam, Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam.
Hatahivyo Kwaupande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Al Bukhar Foundation Sheikh Khalifa Khamisi amewataka Watanzania kipindi hiki cha Mfungo wa Ramadhani kupeleka mawazo na akili kwa wenzetu Wapalestina kwani kwani hawapo katika amani na utulivu.

“Ili tuishi kwa usalama tunaweza kujifunza zaidi katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani Watanzania na Waislamu kwa ujumla sote tupeleke akili zetu na mawazo yetu kwa wenzetu wapalestina, Taifa la Palestina ni taifa ambalo limetekwa, limechukuliwa na Mazayuni (Mayahudi) imewadunisha na kuwadhalilisha Waislamu, Wakristo na Wapalestina wanaoishi katika taifa hilo, wakati sisi tuko hapa katika hali ya amani tukilindwa na askari ambao hawana silaha, wenzetu Wapalestina, Waislamu na Wakristo waishio Palestina wanazungukwa na askari wenye silaha na anaepinga amri anauwawa” Amesema Sheikh Khamisi

Sheikh Khamisi amesema kuwa moja ya leongo la Funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni ili mwanadamu aweze kusalimika na Vishawishi vya Mwili, uweze kuwa na udhibiti tama za mwili na ili muweze kujifunza namna bora zaidi ili Watu waishi kwa Amani.

No comments: