Sheikh Jalala ambae ni
Mmoja wa Viongozi Wakuu wa Waislam Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania
amesema kuwa Kuzaliwa Imam Mah’d (a.t.f.s)
Waislam wote Duniani wanaamini ya kwamba Dunia hawezi Kumalizika mpaka
aje mtu, mtu huyo atakapo kuja atawaokoa wanadamu, kwenye matatizo na dunia
ataibadilisha kuwa kisiwa cha amani, Maelewano, Mshikamano na kuhakikisha dhuma
na Ufisadi unasambaratika duniani.itikadi hii ipo kwenye Dhehebu yote ya
Kiislam.
Hayo aliyasema jana
katika sherehe za kumbukumbu za Kuzaliwa Imam Mahd (a.t.f.s) zikiambatana na ufunguzi wa Maktaba ya “Maarifa”
mbele ya Waandishi wa Habari,Kariakoo Jijini Dar es salaam.
“Haifai na sii sawasawa
kupatikana msomi au sheikh ambae haandiki vitabu, Makala au machapisho mengine
ya kielimu, haifai kwa msomi kutokua na athari za uandishi, ufunguzi huu wa
maktaba leo ni kufungua milango ya kufanya tafiti na kupanua wigo wa elimu, maktaba
hii itumike na watu wa dini zote kupata maarifa na kujisomea kwani maktaba ni
mahala ambapo panamfanya kila msomi kuendana na zama zake na kutambua vizuri
mazingira yake”. Amesema Sheikh Jalala
Aidha Sheikh Jalala alitoa wito kwa jamii nzima ya watanzania
kushikamana na elimu na kuwa utamaduni wa kujisomea kwani kila anaeitaka dunia
basi ni lazima ashikamane na elimu, halkadhalika kila naeitaka akhera lazima
pia ashikamane na elimu.
Shaabn 15 siku mwaka 255 Hijiria alizaliwa Imamu wa 12 wa watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w). Jina lake kamili ni Muhamad, lakini majina yake mengine ni Mahdi, Sahib uz Zaman. Al-Hujjah, baba yake alikuwa Imamu wa 11 Imam Hassan al-Askari (as) na Mama yake alikuwa Nargis Khatoon. Suala la Itikadi ya Imam mahd limekuwa likizua utata mkubwa sana baina ya Madhehebu ya waislamu duniani.