Kiongozi
Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala
amewataka watanzania wasikubali kuridhika na Amani walionayo nchini bali na hatimae wahakikishe amani ya Tanzania inakuwepo
katika nchi zinazopakana na Tanzania
ikiwepo nchi ya Palestina.
“Amani
lazima tuienzi, na tusikubali tukaiacha hapa hapa Amani hii, lazima tuipeleke
kwa wenzetu, lazima tuwaonyeshe wenzetu, lazima tuwaombee Mungu wenzetu
wapalestina na sehemu zinginezo wawe na utulivu kama tulionao. Mungu ibariki
Tanzania, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Palestina, zibariki nchi zote
ambazo hazina utulivu na uzipe amani” Maulana Sheikh Jalala.
Maulana
Sheikh Jalala amesema hayo wakati wa Matembezi ya Amani ya kuadhimisha siku ya
Kimataifa ya Quds, yaliyoanzia katika Viwanja Ilala Boma na kufikizia Viwanja
vya Pipo Kigogo Dar es salaam pamoja na kuhudhuriwa na Waislamu, Wakristo na
Wapenda Amani Tanzania na Ulimwenguni.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mshikamano wa Tanzania na Palestina Mhe. Abdallah Othmani akiongea na Waandishi wa Habari Kigogo Dar es salaam. |
Kwa Upande
wake Mwenyekiti wa Kamati ya Mshikamano wa Tanzania na Palestina Mhe. Abdallah
Othmani ameitaka Serikali kuwa Tuinaimba Serikali yetu izidi kupaza sauti juu
ya swala la Palestina, wapalestina wametoa mchango mkubwa katika afrika,
tusiaache wakiwa, turejee katika maneno ya baba wetu wa Taifa alivyokuwa na
msimamo wake juu ya swala ya Palestina, tuhakikishe ndugu zetu wapalestina,
tunawaunga mkono kwa hali na mali.
“Hatuna
chuki na Waisraeli ni Binadamu kama sisi, ila siasa zile za kupora ardhi, siasa
za uvunjifu wa amani wa haki za Binadamu, hilo ndilo tatizo tunalolisitikia,
kwahivyo tunamuomba Raisi wetu apaze sauti juu ya jambo hili, ili kuwatizama
wapalestina katika jicho la huruma na wao” amesema Mhe. Othmani.
Waumini wa Kiume wa Dini ya Kiislamu wakifanya Matembezi ya Amani ya Kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds, Jijini Dar es salaam |
Waumini wa Kike wa Dini ya Kiislamu wakifanya Matembezi ya Amani ya Kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds, Jijini Dar es salaam |