Kiongozi
Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala amesema
kuwa Imam Khomein (r.a) aliuelewa Uislamu kwamba inawezekana ukaishi katika
dunia tuliokuwa nayo maisha yako yote kuwa ni Maisha ya Kiislamu na ukaishi na
jamii isiyokuwa ya Kiislamu ikakupenda na ikakusikiliza.
Maulana
Sheikh Jalala amesema hayo katika Semina ya Kumbukizi ya Kifo cha Imam Khomein
(r.a), Semina ambayo iliwakusanya Maustadhi, Masheikh na Maimam, iliyofanyika
Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam.
Maulana
Sheikh Jalala amesema kuwa ukijaribu kuisoma historia na Mwenendo wa Imam Khomein (r.a) na mahusiano yake na watu
utaona kuwa ni Bingwa wa Uislamu na Bingwa wa Amani kwani hakuna siku
alilingania Ushia, wala Umadhehebu, wala kundi fulani bali alilingania Laailah
ilallah, Muhammadun Rasulullah.
Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Mhe. Mousa Farhang akiongea na Maustadhi, Masheikh na Maimam katika Semina ya Kifo cha Imam Khomein. |
Kwa upande
wake Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Mhe. Mousa Farhang amesema
kuwa Kumbukumbu ya Imam Khomein (r.a) hakumbukwi kwa ukubwa wake bali
inakumbukwa Fikra na Mitazamo yake nay ale aliyoyafanya akiwa hai, ili
kuyaendeleza kwa Vizazi vijavyo.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Mhe. Abbas Farmand akiongea katika Semina ya kumbukizi ya Kifo cha Imam Khomein. |
Aidha nae
Mkurugenzi wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Mhe.
Abbas Farmand amesema kuwa Maisha ya Imam Khomein (r.a) unaweza kuyaangalia
katika sehemu mbalimbali ya Kielimu, Kisayansi, Kijamii na Kisiasa, katika
Maswala ya Kifamilia utaona hana mfano.
Masheikh, Maimam na Maustadhi waliohudhira katika Semina ya Kumbukizi ya Kifo cha Imam Khomein, Dar es salaam. |
No comments:
Post a Comment