Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana
Sheikh Hemed Jalala amewataka Wajane kujishugulisha kwa kufanya Biashara
mbalimbali za kujiletea maendeleo na kutokata tama ya maisha kwasababu wanae
kiigizo ambaye ni Bi Khadija Mke wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).
“Kitendo cha Bibi Khadija (a.s)
kujishughulisha kufanya Biashara, kuwa Mjasiliamali, kufanya harakati za
uzalishaji ni dalili tosha na ni kiigizwa tosha cha kwamba Mwanamke Mjane,
kumbe anaweza kuwa mjasiliamali, kumbe anaweza kujifanyia Biashara zake
ndogondogo, na kuendesha Maisha yake na watoto alioachiwa na mwenzake” alisema
Sheikh Jalala
Akizungumza Jana na Wajane takriban 350 wa kata ya Kigogo
katika Futari ya pamoja wakati wa
kuadhimisha kumbukumbu ya Kifo cha Bi Khadija (a.s) Mke wa Mtume Muhammad
(s.a.w.w), iliyoandaliwa na Kitengo cha Kinamama wa Chuo cha Imam Swadiq,
iliyofanyika Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam.
Aidha Sheikh
Jalala amewataka Viongozi wa Dini kutumia Misikiti na Makanisa kuwa ni sehemu
ya kuwakusanya wajane na Watanzania bila kujali dini zao kufanya hivyo ni
kujenga Amani, Upendo, Umoja na Mshikamano, Misikiti na Makanisa isitumike
kuwagawa Wajane na Watanzania.
“Leo hii wamekusanyika wajane pasina kubagua dini zao, wajane
waislamu wako hapa, wajane wakristo wako hapa, ni somo nzuri na la kupendeza
kwamba Misikiti yetu, Makanisa yetu yawe ni Sehemu ya kuwakusanya Waislamu,
yawe ni sehemu ya kuwakusanya Wakristo na waka Misikiti yetu na Makanisa yetu
yasiwe ni nyumba ya kuwagawa watanzania wetu” Alisisitiza Sheikh Jalala
Mkurugenzi wa Mtendaji wa Sadeline Heath Care Trust Mhe Sara Emmanuel akizungumza na Wajane takriban 350 wa kata ya Kigogo katika Futari ya pamoja. |
Nae
Mkurugenzi wa Mtendaji wa Sadeline Heath Care Trust Mhe Sara Emmanuel amewataka
Wajane kujiandisha na kuwa wanachama kwenye Chama cha Wajane Tanzania (TAWIA) kwani
kuna fursa nyingi, ukishakuwa mwanachama
kule Miradi mingi ambayo Serikali inatoa inapita kule na fursa nyingi zinapita
kule” Alisema Sara Emmanuel
Mwenyekiti wa Chama cha Wajane Tanzania (TAWIA) Mhe. Mariam Aswile na wajane wenzake katika futari ya pamoja. |
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wajane Tanzania
(TAWIA) Mhe. Mariam Aswile amewatka wajane kutolala na kuhuzinika badala yake
wamtumikie Mungu, kujitoa na kuchichangaya na wajane wenzie ili kutafuta fursa
mbalimbali ambazo zitasaidia Ujane kuwa mwepesi katika maisha ya kila siku.
“Napenda kusema
kwamba, Wajane kama tumevyosikia somo la Ujasiliamali kwamba tusilale, tukakaa,
tukaendelea kuhuzunika, ila tunapidi
kumtumikia Mungu, kujitoa na kujichanganya kama leo tumevyojichanganya
mambo yetu yatakuwa ni Rahisi zaidi, hata huo Ujane utakuwa ni Mwepesi” Alisema
Aswile.
No comments:
Post a Comment