|
RAIS
wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Museveni |
Na Radhia Soud
RAIS
wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Museveni anatarajia kufanya ziara ya
Kitaifa ya siku mbili nchini ambao inalenga kukuza mahusiano mazuri
yaliyopo baina ya Uganda na Tanzania pamoja na kujadili masuala
mbalimbali ya kikanda, kimataifa na maeneo ya ushirikino kati ya nchi
hizi hususani katika maeneo ya Biashara, Nishati,Uchukuzi na yale
yanayohusu ujirani mwema.
Museveni anatarajiwa kuwasili
februari 25 kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa
ni ziara yake ya kwanza nchini tangu kuingia kwa serikali ya hawamu ya
tano.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es salaam
Waziri wa Mambo ya nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Augestine
Mahiga alisema Uganda ni majirani zetu na tuna historia ya pekee nao
kwani tulishapiga vita nao na kumwaga damu kipindi cha Iddi Amini.
"
Mahusiano ya Tanzania na Uganda ni mazuri na yamekuwa yakiimarika kila
mara na kumekuwepo na ziara za mara kwa mara za viondozi wakuu wa
kitaifa wa nchi hizi ikiwemo ziara ya Rais wa Uganda Museveni
alipoudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Magufuli" alisema Mahiga.
Alisema
katika ziara hiyo Rais museveni hatatembelea maeneo mbalimbali ikiwemo
Viwanda vya kampuni ya Said Salim Bakhresa ambaye pia amewekeza nchini
Uganda na baadaye Bandari ya Dar es salaam.
Aliongezea kuwa
nchi ya uganda ina umuhimu mkubwa kwa Tanzania kutokana na jiografia
yake katika Jumuhiya ya Afrika Mashariki na ni nchi isiyokuwa na bandari
hivyo inaitegemea Tanzania Kwa ajili ya kupitisha mizigo yake.
"
Uganda ni nchi ambayo haina bandari na inategemea nchi za jirani
kupitishia mizigo yao ikiwemo Tanzania, lakini kwa mda kidogo bandari
yetu ilikuwa na matatizo na walikuwa wakitumia bandari ya Mombasa lakini
kwa sasa tumeshatatua matatizo hayo" alisema Mahiga
Alisema
nchi hiyo pia imezidi kuwa na umuhimu kufuatia uamuzi wa kupitisha
bomba la mafuta nchini Tanzania, kutokea Kaabale-Hoima, Uganda hadi
Bandari ya Tanga.
Aidha alisema bomba hili linatarajiwa
kukamilika ifikapo mwaka 2020 ambalo lina urefu wa kilometa 1443 na
kipenyo cha nchi 24 ambapo utekelezaji wa mradi huu unategemewa kuwa na
faida nyingi kwa taifa ikiwemo kufungua fursa za ajira kwa watanzania.
Akijibu
swali alilokuwa ameulizwa na Mwandishi wa habari kuhusiana na
watanzania waliofukuzwa msumbiji Waziri Mahiga alisema kuwa Tanzania na
Msumbiji ni chini ambazo zina ushirikiano mzuri wa undugu na kisiasa na
kuhusu matatizo sio tu msumbiji bali wamekuwa na matatizo na nchi
nyingine.
Alisema kuwa watanzania waliofukuzwa msumbiji
walikuwa hawana kibali cha kuishi ndani ya nchi hiyo na walikuwa
wakijiusisha na kazi mbalimbali ndani ya nchi hiyo bila kufuata taratibu
za nchi husika.
" Kama mnakumbuka hapa Tanzania tulikuwa
na operesheni kimbuga ambayo tulikuwa tukiwafukuza wakimbizi waliokuwapo
hasa mipakani mwa nchi yetu lakini wenzetu msumbiji walitumia busara
kwani walitoa mda kwa watanzania kuondoka na mda ulipoisha waliongeza
lakini kuna waliondoka na walibaki lakini bado tunaendelea kulifuatilia"
alisema Mahiga
Hata hivyo aliongezea kuwa siku ya leo
Februari 24 kutakuwa na mkutano utakaowakutanisha mawaziri 15 wa jumuiya
ya SADC ambapo waziri wa msumbiji atakuwepo na watalizungumzia kiundani
zaidi swala hilo.