Thursday, February 23, 2017

Raisi wa Uganda Yoweri Museven atarajia kuwasili Nchini Tanzania kwa ziara ya siku mbili

Image result for museveni
RAIS wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Museveni
Na Radhia Soud

RAIS wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Museveni anatarajia kufanya ziara ya Kitaifa ya siku mbili nchini ambao inalenga kukuza mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Uganda na Tanzania pamoja na kujadili masuala mbalimbali ya kikanda, kimataifa na maeneo ya ushirikino kati ya nchi hizi hususani katika maeneo ya Biashara, Nishati,Uchukuzi na yale yanayohusu ujirani mwema.
Museveni anatarajiwa kuwasili  februari 25 kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni ziara yake ya kwanza nchini tangu kuingia kwa serikali ya hawamu ya tano.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es salaam Waziri wa Mambo ya nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Augestine Mahiga alisema Uganda ni majirani zetu na tuna historia ya pekee nao kwani tulishapiga vita nao na kumwaga damu kipindi cha Iddi Amini.
" Mahusiano ya Tanzania na Uganda ni mazuri na yamekuwa yakiimarika kila mara na kumekuwepo na ziara za mara kwa mara za viondozi wakuu wa kitaifa wa nchi hizi ikiwemo ziara ya Rais wa Uganda Museveni alipoudhuria  sherehe za kuapishwa kwa Rais Magufuli" alisema Mahiga.
Alisema katika ziara hiyo Rais museveni hatatembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Viwanda vya kampuni ya Said Salim Bakhresa ambaye pia amewekeza nchini Uganda na baadaye Bandari ya Dar es salaam.
Aliongezea kuwa nchi ya uganda ina umuhimu mkubwa kwa Tanzania kutokana na jiografia yake katika Jumuhiya ya Afrika Mashariki na ni nchi isiyokuwa na bandari hivyo inaitegemea Tanzania Kwa ajili ya kupitisha mizigo yake.
" Uganda ni nchi ambayo haina bandari na inategemea nchi za jirani kupitishia mizigo yao ikiwemo Tanzania, lakini kwa mda kidogo bandari yetu ilikuwa na matatizo na walikuwa wakitumia bandari ya Mombasa lakini kwa sasa tumeshatatua matatizo hayo" alisema Mahiga
Alisema nchi hiyo pia imezidi kuwa na umuhimu kufuatia uamuzi wa kupitisha bomba la mafuta nchini Tanzania, kutokea Kaabale-Hoima, Uganda hadi Bandari ya Tanga.
Aidha alisema bomba hili linatarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2020 ambalo lina urefu wa kilometa 1443 na kipenyo cha nchi 24 ambapo utekelezaji wa mradi huu unategemewa kuwa na faida nyingi kwa taifa ikiwemo kufungua fursa za ajira kwa watanzania.
Akijibu swali alilokuwa ameulizwa na Mwandishi wa habari kuhusiana na watanzania waliofukuzwa msumbiji Waziri Mahiga alisema  kuwa Tanzania na Msumbiji ni chini ambazo zina ushirikiano mzuri wa undugu na kisiasa na kuhusu matatizo sio tu msumbiji bali wamekuwa na matatizo na nchi nyingine.
Alisema kuwa watanzania waliofukuzwa msumbiji walikuwa hawana kibali cha kuishi ndani ya nchi hiyo na walikuwa wakijiusisha na kazi mbalimbali ndani ya nchi hiyo bila kufuata taratibu za nchi husika.
" Kama mnakumbuka hapa Tanzania tulikuwa na operesheni kimbuga ambayo tulikuwa tukiwafukuza wakimbizi waliokuwapo hasa mipakani mwa nchi yetu lakini wenzetu msumbiji walitumia busara kwani walitoa mda kwa watanzania kuondoka na mda ulipoisha waliongeza lakini kuna waliondoka na walibaki lakini bado tunaendelea kulifuatilia" alisema Mahiga
Hata hivyo aliongezea kuwa siku ya leo Februari 24 kutakuwa na mkutano utakaowakutanisha mawaziri 15 wa jumuiya ya SADC ambapo waziri wa msumbiji atakuwepo na watalizungumzia kiundani zaidi swala hilo. 

No comments: