Monday, May 23, 2016

Sheikh Jalala “Sababu ya Kusheherekea Mazazi ya Imam Mahd (a.t.f.s), Imam Mahd ataijaza Dunia Amani na Maelewano


Kiongozi Mkuu wa Chuo cha Kiislam (Hawzat) Imam Swadiq (a.s) Sheikh Hemed Jalala amesema sababu ya Wafuasi Shia Ithnasheriya Tanzania wanaherekea kuzaliwa Imam Mah’d (a.t.f.s) amabe ni Kiongozi wa 12 baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w).kuwa anatakuja kuijaza Dunia Amani na Maelewano.

Sheikh Jalala ambae ni Mmoja wa Viongozi Wakuu wa Waislam Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania amesema kuwa Kuzaliwa Imam Mah’d (a.t.f.s)  Waislam wote Duniani wanaamini ya kwamba Dunia hawezi Kumalizika mpaka aje mtu, mtu huyo atakapo kuja atawaokoa wanadamu, kwenye matatizo na dunia ataibadilisha kuwa kisiwa cha amani, Maelewano, Mshikamano na kuhakikisha dhuma na Ufisadi unasambaratika duniani.itikadi hii ipo kwenye Dhehebu yote ya Kiislam.

Hayo aliyasema jana katika sherehe za kumbukumbu za Kuzaliwa Imam Mahd (a.t.f.s)  zikiambatana na ufunguzi wa Maktaba ya “Maarifa” mbele ya Waandishi wa Habari,Kariakoo Jijini Dar es salaam.

“Haifai na sii sawasawa kupatikana msomi au sheikh ambae haandiki vitabu, Makala au machapisho mengine ya kielimu, haifai kwa msomi kutokua na athari za uandishi, ufunguzi huu wa maktaba leo ni kufungua milango ya kufanya tafiti na kupanua wigo wa elimu, maktaba hii itumike na watu wa dini zote kupata maarifa na kujisomea kwani maktaba ni mahala ambapo panamfanya kila msomi kuendana na zama zake na kutambua vizuri mazingira yake”. Amesema Sheikh Jalala
Aidha Sheikh Jalala  alitoa wito kwa jamii nzima ya watanzania kushikamana na elimu na kuwa utamaduni wa kujisomea kwani kila anaeitaka dunia basi ni lazima ashikamane na elimu, halkadhalika kila naeitaka akhera lazima pia ashikamane na elimu.

Shaabn 15 siku mwaka 255 Hijiria alizaliwa Imamu wa 12 wa watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w). Jina lake kamili ni Muhamad, lakini majina yake mengine ni Mahdi, Sahib uz Zaman. Al-Hujjah, baba yake alikuwa Imamu wa 11 Imam Hassan al-Askari (as) na Mama yake alikuwa Nargis Khatoon. Suala la Itikadi ya Imam mahd limekuwa likizua utata mkubwa sana baina ya Madhehebu ya waislamu duniani.

No comments: