TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI.
MAADHIMISHO
KIFO CHA MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W) MWEZI 28, SAFAR 1438.
Napenda kuanza na mazungumzo yangu katika Qur’an
Mungu ansema “Hatujakutuma ewe Muhammad (s.a.w.w) ila ni huruma kwa viumbe wote”
siku hii ya leo ya mwezi 28,mfungo tano kwa kalenda ya Hijiria ndio siku ambayo
Kiongozi wa watu wote duniani, kiongozi wa Waislam Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) ndio ameaga dunia.
Weusi huu mnaouona, matembezi haya ya amani
mnayoyaona yote ni kwasababu ya kukumbuka kifo cha mtukufu na mtakatifu Mtume
Muhammad (s.a.w.w), Lakini lakujiuliza kubwa ni kwanini mtu huyu tumkumbuke
katika kifo chake, zaidi ya miaka 1400 iliyopita.
Sababu kubwa ya kukumbuka kifo cha Bwana
Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuna sababu nyingi mmno, lakini niseme sababu mbili
tatu kwa harakaharaka, Sababu ya kwanza kama anavyosema Mwenyezimungu katika
Qur’an kwamba “Wewe tumekutuma ukawe ni huruma kwa watu wote” sio huruma kwa
Waislam,
Sasa unapomuangalia Mtume Muhammad (s.a.w.w)
wakati bado yupo hai, akiwa yuko katika mji wa makka na baada ya kuwa madina,
tulimpata mtume alikuwa na huruma kwa watu wote, mtume alikuwa huruma kwa
wasiokuwa waislam, mtume alikuwa na huruma kwa waislam, mtume alikuwa huruma
kwa wtu waliokuwa wanaabudu masanamu, kwa watu waliokuwa wanaabudu lata,
wanaabudu manata na wanaabudu hubal,
hawa walikuwa ni waungu wakiabudiwa na
warabu, lakini mtume aliishi vizuri na alikuwa ni huruma kwa watu hao, mpaka
amana za watu hao aliziweka katika
nyumba yake,
Mtume alipokuwepo maka na madina vilevule
alikuwa na huruma kwa Ahlulkitab / Wakristo, yaani alikuwa ni huruma kwa
Wakristo, alikuwa na huruma kwa mayahudi na alikuwa ni huruma kwa watu wenye
dini zote.
Naamimi ya kwamba huruma hii aliyokuwa nayo
Mtume Muhammad (s.a.w.w) kabla hajaondoka duniani, naamini ya kwamba Watanzania
na walimwengu huruma hii wanaihitajia.
Leo hii tunapotembea matembezi haya ya amani
kwa ajili ya kukumbuka Mtume Muhammad (s.a.w.w) kifo chake, kubwa la kulienzi
ni hili la Huruma ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) inahitajika na ni muhimu,
Naamini
yakwamba Watanzania wote wanahitajia huruma aliyokuwa nayo mtume, huruma ambayo
haikumfanya Mtume asiwapende wasiokuwa waislam.
Huruma ambayo ilimfanya mtume akae meza moja
na Wakristo katika ardhi ya madina, Huruma ambayo ilimfanya Mtume akae meza
moja na Mayahudi, huruma ambayo ilimfanya Mtume akae na Wakristo / Ahlulkitabu.
Naamini yakwamba leo hii Waislam watanzania
Masheikh na Maimam na Maustadhi wanayonafazi kubwa yakumuenzi Mtume katika
kukaa kwao na Wachungaji, wao na Maaskofu, wao na Mapari, wao na wenzi wao
ambao wanatofautiana nao kidini, Naamini ya kwamba Matembezi haya yawe ni
chachu yakuwafanya watanzania wote waiige huruma ya Mtume,
ambayo huruma hiyo
ilikuwa haimbagui mtu, huruma hii leo hii inahitajika mahala pakubwa.Bwana
Mtume Muhammad (s.a.w.w) alikuwa ni huruma kwa watu wote kwanini kwasababu
alikuwa na huruma na watu.
Jambo la pili Mtume ambae tunamkumbuka leo
hii, ni mtume alieng’ang’ania na alieenzi Umoja kabla ya mtume hajaondoka makka
alitengeneza umoja kati ya maswahaba wake, na alipoondoka makka kwenda madina
vile vile akatengeneza umoja kati ya wakazi wa madina (Answar) na kati ya watu
waliotoka Makka(Muhajirun).
Akatengeneza Umoja kati ya makabila mawili
yaliyokuwa yanavutana kabila la Ausi na Azraj, akatengeneza umoja wa Kidini
ndani ya ardhi ya madina,naamimi ya kwamba leo hii, uwepo wa umoja wa Kidini
ndani ya ardhi ya Tanzania,kipindi hiki ambacho huruma imekosekana ,
kipindi
ambaho kuvumiliana kumekosekana, naamimi ya kwamba mafunzo haya Mtume Muhammad
(s.a.w.w) yanahitajika leo hii kwa Watanzania na watu wote bila ya kuwabagua
waislam wala wakristo wote wanahitajia umoja huu, wanahitajia kuishi huku kwa
pamoja ameyoyafunza Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Nimalizie kwa kusema yoyote ambae anafikra ya
kwamba Uislam ni dini ambayo haina huruma huyo atakuwa hajautambua Uislam, yoyote ambae anafikiria ya kwamba
Mtume alikuwa ni mtu wa Misimamo ya kutisha ambayo hawezi kukaa na watu hayo
hajamtambua Mtume.
“Kwasababu ya huruma uliyokuwa nayo ewe Muhammad (s.a.w.w)
watu wote wameweza kukukubali, umeweza kukaa na Wakristo, umeweza kukaa na
Mayahudi,umeweza kukaa na Mapagani na umeweza kukaa na watu wa aina zote”
Jambo la Mwisho Mtume Muhammad (s.a.w.w) kama
alivyoenzi Umoja, ulienzi utulivu, alienzi maelewano na alienzi amani, na
ninaamini yakwamba Tanzania leo hii inayohaja kubwa yakuenzi Utulivu, yakuenzi
Amani, yakuenzi Mshikamano watu kukaa pamoja, tofauti zetu za kifikra na za
kimtazamo zisitufanye kutokuwa wamoja.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki
wanadini wote walioko Tanzania, wabariki Viongozi wa Dini wahubiri Upendo,
Maelewano, Mshikamano pamoja na Amani katika nchi hii,Vilevile Viongozi wetu na
Serikali ambayo inatusimamia katika mambo yetu.
Imetolewa
na:
Kiongozi
Mkuu wa Waislam Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala
30-11-2016,Jumatano.
No comments:
Post a Comment