Mkuu wa Dawati la Jinsia na
Watoto Mkoa wa Polisi Kinondoni ASP Fatuma Mitarimbo ameitaka jamii ya
Kitanzania kwenda katika Dawati la Jinsia na Watoto ili kupunguza matatizo
mbalimbali yanayosababishwa na Ukatili wa Kijinsia.
“Jeshi
la Polisi nchini lina vituo 417 vya Dawati la jinsia na Watoto Tanzania nzima,
na watu wote wanakaribishwa katika vituo hivyo kuja kutoa taarifa ya matatizo
yao ya Ukatili wa Kijinsia ili matatizo hayo tuweze kuyapunguza katika jamii
yetu” amesema Mitarimbo.
ASP Mitarimbo amesema hayo leo
katika Warsha ya mafuzo kwa Wajane, katika kuadhimisha siku ya 16 za kupinga
Ukatili wa Kijinsia, katika Mtaa wa Udoe (Masjid Udoe), Bilal Muslim Mission of
Tanzania, Kariakoo Dar es salaam.
Warsha hiyo iliandaliwa na Chama
cha Wajane Tanzania / Tanzania Widows Association (TAWIA), ikishirikiana na WilDAF
pamoja na Bilal Muslim Mission of Tanzania. ikiwa na Kauli mbiu"Funguka,
pinga Ukatili wa Kijinsia, Elimu salama kwa wote"
Kuna
aina kuu nne ya Ukatili wa jinsia ambayo ni Ukatili wa Mwili, ukatili wa Kisaikolojia,
ukatili wa Kingono na ukatili wa Kiuchumi. “katili wa Kijinsia ni Kitendo
chochote kinachoweza kumsababishia mtu mwingine kuwa na madhara, madhara hayo
yanaweza kuwa madhara ya kimwili, kingono, kisaikolojia na Kiuchumi” amesema
Mitarimbo
Aidha ASP Mitarmbo ametoa wito kwa
Jamii kutoa taarifa katika Jeshi Polisi
kitengo cha Dawati la jinsia na Watoto, Misikitini, Makanisani, kwa Viongozi wa
Dini na taasisi zinazohusika na kuzuia na kupambana na Ukatili wa Kijinsia ili
kupunguza ukatili nchini" amesema ASP Mitarimbo
Chimbuko
la kuadhimisha siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia ni kutokana na mauaji ya
kinyama kwa akina dada watatu ambao ni wa Kilamabela ambao walikuwa wanaishi
katika nchi ya Dominika, waliuuwa mwaka 1960, chanzo cha kuuwawa kilisababishwa
na Wanaume zao ambao walikuwa wanapinga uongozi wa mbaya wa kiongozi wao
Leonard Tujilo.
Kwa
upande wa Jeshi la Polisi Tanzania tangu mwaka 2009, Jeshi la Polisi liliona
kwamba ukatili wa Kijinsia umeshika usikani/ unakuwa, ukatili wa kijinsia ukawa
ni chanzo cha makosa, ni chanzo cha watoto wetu kuzagaa mitaani, ni chanzo cha
ndoa nyingi kutengana/kuvunjika na ni chanzo kikubwa sana cha kupoteza baadhi
ya vioungo.
Hapo
jeshi la polisi likasema hapana, likawa linatafuta namna ya kupunguza vitendo
kama hivi, kwani mara nyingi vitendo kama hivyo vinafanyika kwa siri,hivyo
jeshi la polisi likaona umuhimu wa kufungua Dawati la jinsia na watoto ili
kuwapa nafasi akina mama, baba na watoto kuja kulalamika na kutoa dukuduku lao
na kunapolisi ambao wamefundishwa vizuri na hawawezi kuja kutoa siri.
|
No comments:
Post a Comment