Kiongozi Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheriya Duniani Ayatullah Sayyid Ali Khamenei. |
Kiongozi Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheriya Duniani Ayatullah Sayyid Ali Khamenei
ametuma ujumbe kwa jumuiya za Kiislamu za wanafunzi wa vyuo vikuu barani
Ulaya na kusema: "Ni jukumu la kila mtu kupeperusha bendera ya Uislamu
halisi katika vita visivyo na usawa vya makabiliano na mrengo wa kufru
na uistikbari."
Ayatullah Sayyed Ali Khamenei, katika ujumbe wake huo
uliotolewa Ijumaa hii, amesema: "Ni matarajio yangu kuwa mbali na kuwa
mtajijenga kielimu, kidini na kiakhlaqi, muwe pia ni wenye taathira
katika mazingira yenu na muongoze watu zaidi wafuate njia ya Mwenyezi
Mungu kwa maneno na vitendo vyenu vyema."
Ayatullah Khamenei ameashiria kuwa,
'ujana na uanachuo' ni nukta zenye nguvu ambazo humsaidia mwanadamu
kufikia malengo yake ya juu' na kuongeza kuwa, 'mbali na kuwa muna sifa
hizo mbili, pia mna sifa nyingine yenye taathira nayo ni kupitia jumuiya
za Kiislamu.'
Kiongozi amesisitiza kuwa, kila moja anapaswa kunufaika na baraka za
chemchemu ya maarifa sahihi ya Kiislamu na kuwa katika njia nyofu ya
Mwenyezi Mungu.
No comments:
Post a Comment