Vitendo vya makosa ya ukatili wa kijinsia na watoto vimezidi kuongezeka katika wilaya ya Ilala hadi kufikia 208 tofauti na mwaka jana ambapo takwimu zilikuwa chini kwa makosa 168.
Unyanyasaji huo unajitokeza
katika sura mbalimbali kama vile vipigo,ukeketaji,ubakaji,mauaji ya wanawake na
watoto wa kike,kurithi wajane pamoja na ukatili wa nyumbani.
Kauli hiyo
ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Kaimu Kamanda wa
Mkoa wa Ilala ambaye pia ni mkuu wa upelelezi mkoa wa
kipolisi Ilala, Juma Bwire, wakati alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na vitendo
vya kikatili wa kijinsia wanavyofanyiwa wanawake
na watoto.
Kamanda Bwire amesema kutokana na vitendo vya kikatili
kuzidi kuongezeka, Jeshi la Polisi limekuja na mkakati
endelevu kwa ajili ya kuwasaidia
waathirika wa vitendo hivyo ambapo leo watanzidua kituo cha
kulelela watoto waishio katika mazingira hatarishi.
Amesema kuwa huduma
katika kituo hicho zitatolewa na wataalamu waliopata mafunzo ya
kutosha ili kuweza kutatua kero zinazohusiana na
masuala ya kijinsia na suluhisho la muathirika litatatuliwa
na kupatiwa ufumbuzi wa pamoja kwani huduma zote za
kipolisi zitapatikana hapo katika kituo hicho.
Hatahivyo amesema katika kuadhimisha siku 16 za ukatili wa
kijinsia leo kutakuwa na maandamano ambayo yataanzia katika Ofisi
ya Kipolisi Mkoa wa Ilala na kumalizikia Viwanja
ya mnazi mmoja.
No comments:
Post a Comment