|
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akisalimiana na Viongozi wa Hawzat Imam Swadiq (a.) katika Sherehe za Kumbukumbu za Mtume Muhammad (s.a.w.w). |
|
|
|
Kumbukumbu hizo zimefanyika leo usiku katika viwanja vya Kigogo Roud About, jijini Dar es salaam, iliyoandaliwa na Waislam wa Dhehebu la Sunni.
|
Mwalim Mkuu wa Chuo cha Kiislam cha Misri hapa Dar es salaam, Tanzania akitoa hotuba ilisotoa sifa kwa Mkoa wa Dar es salaam,kuwa ni Mkoa wenye kumpenda sana Mtume Muhammad (s.a.w.w) |
|
Maulana Sheikh Hemed Jalala akitoa hotuba yake iliyoaanza kwa kuuliza "Madrasa ni nini" mbele ya Waumini wa Dini ya Kiislam. |
“Taifa hili kama lina hitajia kuifunga Taasisi ya Takukuru, kupata
wakusanyaji kodi wazuri, rai wema na wasio waovu, na wala Rushwa basi ni
kuzienzi madrasa, na akaitaka wizara ya elimu kuzienzi madrasa hizo na
kuzitia nguvu kwa kuzipa posho kwani kazi zinazofanya zina mchango
mkubwa kwa jamii na kwa Taifa kwa ujumla." Amesema Sheikh Jalala.
Aidha Maulana Hemed
Jalala ametoa wito kwa Taifa la Tanzania kama linahitaji watumishi wenye
maadili mema ni lazima kuzienzi Madrasa.
|
Hawa ni baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislam wakiume wakiwa makini katika kusikiliza Sifa na Mashairi mbalimbali za Kumsifu Mtume Muhaammad (s.a.w.w) |
No comments:
Post a Comment