Wataalamu na wanasheria wamesema kuna udharura wa kuundwa "jopo la
waamuzi" la kufuatilia maafa ya Mina. Abbas Ali Kadkhodai, mhadhiri wa
Taaluma ya Sheria wa Chuo Kikuu cha Tehran amesema maafa ya Mina
yameweka wazi suala la mas-ulia ya viongozi wa Saudi Arabia kwa sababu
ima kuna uzembe au kosa la makusudi lililofanywa katika maafa hayo.
Akizungumza katika majadiliano maalumu ya kuzungumzia kadhia ya Mina,
mhadhiri huyo wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Tehran ameongeza kuwa
katika sheria za kimataifa serikali zina jukumu la kulinda raia wa
kigeni na mas-ulia ya kudhamini usalama wa maisha yao.
Mehdi Davatgari,
mtaalamu wa sheria na mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Usalama wa Taifa na
Sera za Nje amesema kuhusiana na maafa ya Mina kuwa mbali na suala la
kuundwa kamati ya kutafuta ukweli itakayoweza kuchunguza nukta
mbalimbali kuhusiana na maafa hayo, kufidia hasara ndiko kunakoufanya
utawala wa Aal Saud uwe na mas-ulia juu ya kadhia hiyo.
Fadhlullah
Musavi, mkuu wa zamani wa kitengo cha Sheria na Sayansi ya Siasa cha
Chuo Kikuu cha Tehran amesema kamati ya kutafuta ukweli kwa ajili ya
kufuatilia maafa ya Mina inapasa iundwe na Umoja wa Mataifa.
Amefafanua
kuwa utendaji dhaifu wa serikali ya Saudia katika maafa ya Mina
unalifanya liwe na udharura na ulazima suala la uundaji kamati ya
kimataifa ya kutafuta ukweli kwa ajili ya kufuatilia maafa hayo.chanzo irib
No comments:
Post a Comment