Rais Vladimir Putin wa Russia amesema
mashambulizi ya anga ya jeshi la nchi yake dhidi ya magaidi nchini Syria
yamekuwa na matokeo mazuri tangu yalipoanza na kwamba serikali na jeshi
la nchi yake litaendelea kuiunga mkono serikali halali ya Damascus.
Akizungumza kwenye mahojiano na kanali moja ya televisheni nchini
Russia, Rais Putin amesema kuwa hakuwezi kufanyika mazungumzo ya amani
kwa ajili ya kutatua mgogoro wa Syria ilihali bado makundi ya kigaidi
yanaendelea kushambulia raia. Hii ni katika hali ambayo ripoti
zinaonyesha kuwa, jeshi la Syria likisaidiwa na ndege za kivita za
Russia limeweza kuwarudisha nyuma magaidi na kudhibiti maeneo kadhaa
katika mkoa wa Hama, magharibi mwa nchi.
Huku hayo yakijiri, Mawaziri wa Mambo ya
Nje wa nchi za Umoja wa Ulaya mapema leo wametoa taarifa ya kukosoa
hatua ya Russia ya kushambulia ngome za magaidi nchini Syria. Taarifa
hiyo iliyotolewa baada ya mkutano wa mawazi hao huko Luxemburg imesema
Russia inalenga kudhoofisha wapinzani wa Syria badala ya kupambana na
magaidi. Tuhuma hizo za EU zimekanushwa vikali na serikali ya Moscow.chanzo irib
No comments:
Post a Comment