Mjumbe wa Baraza Kuu la Mapinduzi ya Yemen Bwana Abdur Rahman Mukhtar
amesema kuwa Israel inashirikiana na Saudi Arabia kufanya ujasusi nchini
Yemen na kwamba ndege za kivita za pande hizo mbili zinashambulia kwa
pamoja maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.
Amesema kuwa Saudi Arabia
imeshambulia maeneo mawili ya Yemen kwa kutumia silaha ambazo Mashariki
ya Kati hazipatikani katika nchi yoyote isipokuwa katika utawala ghasibu
wa Israel. Ameongeza kuwa mmoja wa maafisa wa zamani wa ngazi za juu wa
Saudia aliyefanya safari huko Tel Aviv amemshukuru Waziri Mkuu wa
Israel, Benjamin Netanyahu kwa kuupa utawala wa Riyadh silaha za aina
hiyo.
Saudi Arabia na waitifaki wake tarehe 26 Machi mwaka huu walianzisha mashambulizi makali dhidi ya taifa la Yemen kwa kisingizio cha kumrejesha madarakani rais aliyetoroka nchi. Miongoni mwa jinai kubwa za Saudi Arabia huko Yemen ni kuushirikisha moja kwa moja utawala wa Kizayuni wa Israel katika mashambulizi ya anga, nchi kavu na majini dhidi ya Waislamu wa Yemen.
Siku chache zilizopita uongozi wa Jeshi na Kamati za Wananchi wa Yemen ulitangaza kuwa una habari za kushiriki moja kwa moja utawala wa Kizayuni wa Israel katika mashambulizi ya anga, nchi kavu na baharini katika muungano wa Saudia dhidi ya eneo la Bab al Mandab.
Wakati huo huo Mkuu wa majeshi ya Israel alisema siku chache zilizopita katika Taasisi ya Siasa za Mashariki ya Kati mjini Washington huko Marekani kwamba jeshi la utawala huo linatilia maanani eneo la Babul Mandab.
Lango la Babul Mandab ni njia kuu ya baharini kutoka Asia kuelekea Ulaya na Marekani na lina umuhimu mkubwa sana kwa uchumi wa dunia hususan kwa nchi na madola makubwa.

Katika upande wa
pili vita vinavyopiganwa na Saudia kwa niaba ya nchi nyingine vinapaswa
kutazamwa katika fremu ya mipango na njama kabambe za Marekani na
Wazayuni katika eneo la Mashariki ya Kati. Kwa msingi huo vita vya Yemen
ni mwanzo wa mpango wa Marekani na waitifaki wake wa kuigawa nchi hiyo
na baadaye nchi za Iraq, Syria, Misri na huenda hata Saudi Arabia
yenyewe.
Njama na mipango hiyo ya Marekani inaonesha kuwa nchi hiyo ingali inafuatilia siasa zake za kikoloni na kujuba zinazofanyika chini ya majina ya Mashariki ya Kati Kubwa au Mashariki ya Kati Mpya ambayo miongoni mwa vielelezo vyake vikuu ni kuzigawa nchi nyingi za eneo hilo na kutimiza ndoto ya Israel ya kuunda dola la Kiyahudi ambalo mipaka yake ni kuanzia mto Nile hadi Furati (Euphrates).
Kwa mijibu wa ramani zilizotolewa hadi sasa kuhusu mpango wa Mashariki ya Kati Kubwa, Yemen ni miongoni mwa nchi zinazolengwa katika mpango huo. Kwa msingi huo ili kuweza kufikia malengo yao huko Yemen, Wamarekani wanatumia fursa zote na wanawaona watawala wa kifalme wa kizazi cha Aal Saud kuwa ndio wenzo na chombo bora zaidi cha kutumia katika vita vinavyopiganwa huko Yemen kwa niaba ya Marekani na Israel.
Jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa nchi za Kiarabu nazo badala ya kuisadia nchi ya Yemen kwa ajili ya kutatua mgogoro wa sasa, zimejiunga Aal Saud katika kutekeleza mipango ya Kimarekani na Kizayuni ya kutaka kuzidhoofisha nchi za Kiislamu za Mashariki ya Kati.
Mashambulizi ya kigaidi na harakati za kiadui za kizazi cha Aal Saud katika kanda hii vinaonesha kuwa nchi zinazohitilafiana au kupinga siasa za Marekani na Israel ndizo zinazolengwa na kukumbwa zaidi na mashambulizi ya kigaidi ya makundi ya kitakfiri na Kiwahabi. Kwa msingi huo kuna ulazima wa Waislamu kuwa macho na makini zaidi mbele ya njama hizo chafu.chanzo irib
No comments:
Post a Comment