Kiongozi wa Waislam Shia Ithnasheriya Maulana Sheikh Hemed Jalala akiongea na Waandishi wa Habari katika Semina ya Maimam kuelekea Siku ya Kimataifa ya Quds, Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam. |
Kiongozi wa
Waislam Shia Ithnasheriya Maulana Sheikh Hemed Jalala amewataka Waislam,
Wakristo, Mayahudi na Watanzania kuwa kitu kimoja katika kuipigania Mashariki ya
Kati ikiwepo Palestina na sehemu zinginezo kuwa katika Amani na Salama.
“Siku hii ya
leo (Ijumaa ya Mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani) ndugu zangu Waislam na
wasiokuwa Waislamu kama tunavyokumbuka Qibla cha Kwanza vilevile tunakumbuka
ardhi ya Mashariki ya kati ikiwemo na Palestina ni ardhi iliyobarikiwa , ni
ardhi yenye Baraka, kwanini ni ardhi yenye Baraka? Ni kwa sababu Mitume
tunaowatambua sisi wametokea pale mashariki ya Kati, ni sehemu inayotuhusu, ni
sehemu inayowahusu Waislamu, Wakristo na Mayahudi” Sheikh Jalala amesema
Sheikh
Jalala amesema hayo katika Semina ya Maimam na Masheikh baadhi wa Mkoa wa Dar
es salaam katika kukumbuka Siku ya Kimataifa ya Quds, ambayo huwa kilele chake
huwa siku ya Ijumaa ya Mwisho katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Masjid Ghadir
Kigogo Post Dar es salaam.
“Sisi
tunambue yakwamba kama waislam kumbe Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) anatokea
sehemu moja,kwahiyo sote waislam ni kitu Kimoja, kama nabii Issa/ Yesu Kristo
(a.s) kwa ndugu zetu wakristo wao ndio Kiongozi wao, Nabii Mussa / Mosses (a.s)
ndugu zetu Mayahudi ndio Kiongozi wao, hawa wote wanatokea Mashariki ya kati,
hii inamaana Quds au Palestina inaweza kutukusanya watu wote wa dini tatu
tukawa kitu kimoja”.Sheikh Jalala amesema.
“Sisi hapa
Tanzania tunajulikana ni Kisiwa cha Amani, Watanzania tunajulikana ni watu
hatubaguani kwa dini zetu tunaishi kama watanzania, lakini ndugu zangu hili la
Amani halipo katika ardhi ya Palestina, halipo Libiya, halipo Syria halipo
sehemu zinginezo ni wajibu wetu kuyakumbuka ya wenzetu, kuwaombea Mungu na
kutaka yatatuke ili na wao wabakie katika salama na Amani kama tulivyobakia
sisi” Sheikh Jalala amesema.
No comments:
Post a Comment