"Leo
tarehe 6 Agosti, 2015 Profesa Ibrahim Lipumba aliitisha mkutano na
waandishi wa habari katika Hoteli ya Peacock, mjini Dar es Salaam na kutangaza kwamba amejizulu nafasi yake kama Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF).
Sisi kama Chama tumezipokea taarifa hizo na tunayaheshimu maamuzi yake.
Ni haki yake ya kikatiba na haki ya kidemokrasia kufanya maamuzi
anayoyaona yana maslahi kwake.
Bila shaka, Profesa Ibrahim
Lipumba amekifanyia kazi kubwa Chama chetu katika miaka 16 ambayo
alikuwa Mwenyekiti wetu, nafasi iliyomfanya awe kiongozi wetu mkuu. Kwa
nafasi yake hiyo, pia ametoa mchango mkubwa katika ujenzi wa demokrasia
katika nchi yetu. Tunaithamini kazi hiyo na tutaendelea kumheshimu kwa
utumishi wake mkubwa kwa Chama chetu na nchi yetu. Tunamtakia kila la
kheri katika mipango yake ya baadaye.
Chama Cha Wananchi (CUF) ni
taasisi na kinaendeshwa kitaasisi. Ndiyo maana maamuzi yake yote
yamekuwa yakifanywa kitaasisi kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama.
Kwa msingi huo, pamoja na ukweli kwamba kuondoka kwa Profesa Lipumba
katika safu ya uongozi kutaacha pengo hasa katika kipindi hichi ambacho
tunaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu, tunawahakikishia wanachama na wapenzi
wa CUF na wananchi wa Tanzania kwa ujumla kwamba Chama hichi hakitayumba
No comments:
Post a Comment