Utawala wa Kizayuni wa Israel umepinga kufanyika
uchunguzi kuhusu mauaji ya Wapalestina yaliyofanywa na jeshi la utawala huo
katika vita vya siku 50 dhidi ya Ukanda wa Gaza.
Danny Eifruni, mwendesha
mashtaka mkuu wa jeshi la utawala wa Kizayuni ameliambia gazeti la Kizayuni la
Haretz kuwa wanapinga kufunguliwa faili la uchunguzi kuhusu mauaji ya raia wa
Palestina yaliyofanywa na wanajeshi wa Israel katika vita vya siku 50 vya mwaka
uliopita dhidi ya Ukanda wa Gaza.
Katika vita hivyo vya mwezi Julai mwaka 2014,
zaidi ya Wapalestina 2,300 waliuliwa shahidi na zaidi ya wengine elfu 11
walijeruhiwa, wengi miongoni mwao wakiwa ni wanawake na watoto.
Wakati huohuo harakati ya Jihadul Islami ya
Palestina imesisitiza kuwa muqawama dhidi ya utawala wa Kizayuni utaendelea,
lengo likiwa ni kuzikomboa ardhi zote za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.
Sheikh Bassam as Saadi, mmoja wa maafisa waandamizi wa harakati ya Jihadul
Islami ametoa sisitizo hilo kufuatia kuuawa shahidi Wapalestina wawili katika
shambulio la hapo jana la askari wa utawala haramu wa Israel huko Ufukwe wa
Magharibi wa Mto Jordan.
Amesema, taifa la Palestina halitoiacha amana ya
Jihadi na muqawama bali litaendeleza harakati na njia ya mashahidi…/
No comments:
Post a Comment