Tuesday, May 26, 2020

“Mzalendo ni Mtu ambae siku zote mtazamo wake ni hapa Kazi tu” Sheikh Jalala

Kiongozi wa Waislamu Shia Ithnasheriya Maulana Sheikh Hemed Jalala akionyesha ishara ya Matumizi ya Akili, na kusema kuwa Ugonjwa wa Corona ileleta Uhuru wa Kufikiri, juzi masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam.
Kiongozi wa Waislam Shia Ithnasheriya Maulana Sheikh Hemed Jalala amesema kuwa Ugonjwa wa Covid 19 umeleta Uhuru kwa bara la Afrika ikiwemo Tanzania kwa kuanza tafiti za Kutafuta dawa na ishara za Uzalendo na badala ya kutomsubiria Shirika la Dawa Duniani.

“Uhuru wa Kufikiria imeletwa na Balaa hili la Ugonjwa wa Corona, Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) wamepata dawa, haya ni maendeleo makubwa hawa ni watafiti wetu wa ndani ya nchi, nah ii ndio dalili ya Uzalendo, mzalendo ni Yule ambae hataki kunyanyua mikono akaomba omba, mzalendo ni Yule ambae mtizamo wake siku zote ni hapa kazi tu, hakuna kuomba omba watu” Sheikh Jalala amesema.

Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania (TIC) Sheikh Abdallah Seif akiongoza Swala ya Eid al Fitiri, Juzi Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam.
Sheikh Jalala amesema hayo wakati akiongea na Waumini wa Dini ya Kiislam katika Khutba ya Swala ya Eid al Fitiri, iliyoswaliwa Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam.

“Jumuiya ya Afrika Mashiriki Viongozi wake wanawasiliana mara kwa mara kuzungumza ni namna gani tutatatua tatizo hili la Ugonjwa wa Corona, mtazamo huu wa waafrika wenyewe na uhuru wa kuangalia wenyewe na maraisi wetu, mtazamo huu kwa kuufanya wao wenyewe ni na uhakika afrika itaondoka na balaa la Umasikini, balaa la Omba omba na balaa na Ubungufu wa Bajeti zao” Sheikh Jalala amesema.

" Tutakuwa sisi ni wachache wa Fadhila, tutakuwa sisi hatujatenda haki kwamba kwa Uhuru wa Fikra na Mtizamo kama hatukumtaja Kiongozi wa nchi yetu Mhe. John Pombe Magufuli, kwa mtizamo wake na uzalendo aliokuwa nao lakini na msimamo ambao leo dunia inauzungumza kwamba ni msimamo wa Kishujaa na ni msimamo wa Kiume katika Vita dhidi ya Ugonjwa wa Corona" Sheikh Jalala amesema.




No comments: