Wednesday, July 27, 2016

Bill Clinton: "Rafiki yangu" Hillary anafaa kuwa rais

Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton amemsifu sana mkewe Hillary na kusema anafaa kuongoza taifa hilo.
Ameambia kongamano kuu la chama cha Democratic mjini Philadelphia kwamba mkewe ndiye “mfumaji bora zaidi niliyewahi kukutana naye”.

Kwenye hotuba yenye hisia kali, amemweleza Hillary kama “rafiki mkubwa” na akasimulia walivyokutana na jinsi anavyojitolea katika utumishi wa umma.

Saa chache awali, mkewe aliibuka kuwa mwanamke wa kwanza nchini Marekani kuidhinishwa kuwania urais na chama kikubwa
Bi Clinton alihitimisha shughuli za usiku huo wa Jumanne kwa ujumbe wa video ambapo alisema: “Siamini kwamba tumefanikiwa kuweka ufa mkubwa zaidi katika dari hili la kioo”, akirejelea hotuba ya mkewe Rais Barack Obama, Michelle, siku ya kwanza ya kongamano.

“Na iwapo kuna wasichana wadogo huko ambao hawajalala na wananitazama, ningependa kuwaambia, huenda nikawa rais wa kwanza mwanamke Marekani na mmoja wenu anaweza kunifuata.”
Awali, Bi Clinton alisimulia walivyokutana katika Chuo cha Uanasheria Yale mwaka 1971.chanzo:bbc

No comments: