Papa Francis ameidhinisha kuundwa
kwa idara mpya itakayokuwa na mamlaka ya kuwawajibisha maaskofu wa
kanisa katoliki wanaokosa kuwachukulia hatua wale waliochini ya
usimamizi wao, wanaotuhumiwa kuwanyanyasa watoto kingono .
Mabadiliko hayo yanafanyika baada ya malalamiko mengi kutolewa na waathiriwa wa vitendo hivyo dhalimu.
Jopo la viongozi wa kanisa hilo pia walikuwa wamependekeza hilo.
Sheria
za dini hiyo, ziitwazo Canon law zilikuwa zimetoa mwongozo wa hatua
gani zichukuliwe dhidi ya maaskofu wanaotelekeza wajibu wao lakini
uongozi wa Vatican haujawachukulia hatua wale wanaofumbia macho makosa
ya unyanyasaji wa kingono unaofanyika katika maeneo yao
Chanzo BBC
No comments:
Post a Comment