Umoja wa Mataifa umetangaza kwamba maelfu ya wananchi wa
Yemen wameuawa katika mshambulizi yanayoendelea kufanywa na Suadi Arabia dhidi
ya nchi hiyo.
Maiti za Watoto wa Nchini Yemen waliouwawa na Saudia Arabic. |
Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Johannes Van Der Klaauw, amesema kuwa mashambulizi ya Saudia huko Yemen yameathiri maeneo yote ya nchi hiyo.
Van Der Klaauw amesema kuwa, Umoja wa Mataifa unataka kupeleka vikosi
vyake nchini Yemen haraka iwezekanavyo.
Ameongeza kuwa kabla ya mashambulizi ya
siku chache za hivi karibuni ya Saudia huko Yemen raia zaidi ya laki tatu
walikuwa wamekimbi makazi yao na ametahadharisha kuhusu mgogoro mkubwa wa
kibinadamu nchini humo.
Shirika la Afya Dunia (WHO) pia limetangaza kuwa tangu tarehe 19 Machi hadi 20 Aprili raia wasiopungua 1080 wakiwemo wanawake na watoto wadogo wa Yemen wameua katika mashambulizi yanayoendelea kufanywa na Saudia dhidi ya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment