Tuesday, July 14, 2015

Jambo la Palestina ni Jambo la Ubinaadamu-Sheikh Hemed Jalala.

Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Mawlana Sheikh Hemed Jalala akiongea na Vyombo vya Habarileo  jijini Dar es salaam

 Habari Kamili

Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala amesema kuwa Jambo la Palestina ni Jambo la Ubinaadamu, matatizo wanayowakumba ni kwa watu wote bila kujali dini zao.
“Jambo muhimu la Paletina ni kuuwaunganisha Waislam na Wakristo Duniani na kusema kuwa jambo la Palestina sio jambo la Kidini bali ni jambo la kila mtu mpenda amani na utulivu na maelewano ya Kibinaadamu.” amesema Sheikh Jalala.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam wakati akiongea na Waandishi wa Habari juu ya Siku ya Kimataifa ya Quds, ambayo huwadhimishwa kila siku ya Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
“Sisi kama Viongozi wa Dini tumeshaanza harakati kabambe za kuwatembelea baadhi za Maskofu, Wachungaji, makanisani kwao lengo la kuwatembelea Maskofu pamoja na Wachungaji ni kuleta Ukaribu na kuwafundisha watanzania kwamba Uislam hausemi ya kwamba Mkristo ni Adui yetu, bali Uislam unasema Mkristo ni ndugu yetu”amesema Sheikh Jalala.
Aidha Sheikh Jalala amesema Qur’an imetamka waziwazi kwamba watu waliokaribu mno na waislam ni wale waliuosema sisi ni wakristo.



No comments: