Saturday, October 10, 2015

NATO yajiandaa kuwatetea waasi nchini Syria na kukabiliana na majeshi ya Urusi

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Katibu mkuu wa Jumuiya ya kujihami ya NATO Jens Stoltenberg amesema Jumuiya hiyo inayoongozwa na Marekani imekamilisha mipango ya  kikosi cha hatua ya haraka cha  hadi wanajeshi 40,000 , mara mbili zaidi ya idadi ya sasa, pamoja na ofisi mapya za makaao makuu ya NATO nchini Hungary na Slovakia. Uamuzi huo umechukuliwa katika mkutano wa Mawaziri wa ulinzi wa NATO leo mjini Brussels, ambao uligubikwa na  wasiwasi wa hatua za kijeshi za Urusi hivi karibuni nchini Syria. Kwani jumuia hiyo imekuwa ikiwaunga mkono waasi na magaidi wanaofanya jinai nchini Syria na Iraq kwa malengo yao machafu ya kisiasa.
Alisema uamuzi huo unatuma ujumbe kwa raia  wote wa nchi za NATO  kwamba Jumuiya hiyo itawalinda, ipo na iko tayari. Akizungumza hapo kabla kuhusu kujiingiza kijeshi Urusi nchini Syria, alisema  Urusi haiwashambulii tu  waasi wa Dola la Kiislamu lakini pia makundi mengine ya waasi na magaidi yanayoungwa mkono na jumuia hiyo yanayoupinga utawala wa Assad . Stolenberg akatoa wito kwa Urusi akisema:
"Ninatoa wito kwa Urusi  itowe mchango madhubuti na wa ushirikiano katika vita dhidi ya magaidi wa Daesh tu na sio kuendelea kuwaua magaidi wa vikundi vingine na kuunga mkono utawala wa Assad. Kwa sababu huo  sio mchango madhubuti kuelekea suluhisho la amani na la kudumu nchini Syria."chanzo abna24

No comments: