Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya
siasa amesema Saudi Arabia inawajibika kulinda usalama wa Mahujaji wa
Nyumba ya Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
Dakta Ali Akbar Velayati amesema kuwa Iran itafuatilia kisheria kadhia ya wahusika wa maafa yaliyotokea Mina nchini Saudi Arabia wakati wa ibada ya Hija na kuongeza kuwa, Riyadh inawajibika kushirikiana na kamati ya kuchunguza ukweli ili kubaini sababu cha maafa hayo na nani walizembea au kusababisha vifo vya maelfu ya Mahujaji.

Amesisitiza kuwa wahusika wa
maafa hayo wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria.
Amesema kwa mujibu wa misingi ya Kiislamu na kibinadamu na vilevile makubaliano ya Vienna nchi mwenyeji inapaswa kulinda usalama wa wageni hivyo Saudia inapaswa kuwajibika katika suala la maafa ya Mina.

Dakta Velayati
amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu italifuatilia suala hilo na maafa
ya Mina kisheria. Maelfu ya Mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu kutoka
pembe mbalimbali za dunia wakiwemo mahujaji 465 wa Iran walifariki dunia
katika mkanyagano uliotokea Mina, Saudi Arabia katika siku ya Idul
Adh'ha wakati wa ibada ya kumpiga mawe shetani.chanzo irib
No comments:
Post a Comment