Tuesday, September 8, 2015

Yajue Maana ya Majina ya Makka Katika Qur'an na Sunna-Sheikh Hemed Jalala 2



 
Mmoja wa Viongozi Wakuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala
Vile vile unaweza kusoma suratul Shuraa aya 7 “Na hiki ni kitabu tulicho kiteremsha  kilicho barikiwa  kinachosadikisha yale yaliyokuwa mbele zako, yaliokuwa mbele yake na kitabu hiki ambacho ni Qur’an ni kwaajili ya kuwahofisha watu wanaokaa kwenye mji unaoitwa Ummul Quran a wale wanaoishi kandokando ya Ummul Quraa wale walioamini akhera wanaiamini na waojuu ya swala zao ni wenye kuzichunga”
Aya inazungumzia nini? Aya hii inatidhibitishia  na kutueleza ya kwamba moja  katika majina ya mji mtakatifu wa makka ambapo mahujaji siku chache zijazo watashuka na kuporomoka katika mji huo, mwenyezimungu(swt) ameuita vilevile ndani ya qur’an Ummul Quraa( mama wa Vijiji).
Kama kuna kijiji kinafaghari kubwa kinaweza kukusanya kila aina ya faghari basi kijiji cha Makka, kijiji kilichopo katika bonde takatifu la Bakka,kijiji hicho ni kijiji ambacho hakina mfano wake, kijiji hicho ni Ummul Quraa(Mama wa Vijiji).
Suratul Fatihi 24, “Na Yeye ndiye aliyeizuia mikono yao kwenu, na mikono yenu kwao, katika bonde la Makka baada ya kukupeni Ushindi juu yao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona myatendayo”
Aya inazungumza mwenyezimungu vipi amewanusuru waislam na kuwasaidia waislam na kuwaunga mkono waislam, lakini hayo yametokea wapi? Yametokea katikati ya mji wa makka.
Aya hizi tatu zinatuwekea barabara ya kwamba Makka inamajina mengi yaliyoitwa ndani ya Qur’an katika majina hayo ni Bakka,Makka na Ummul Quraa ( Mama wa Vijiji), aya hizi zinamaelezo marefu lakini kwa kuwa nipo katika maelekezo na katika darsa ya kubainisha majina ya makka sitoingia kuzisherehesha aya hizo kwa kirefu.
Napenda tuingie katika Sunna katika Riwayat tuziulize riwayat makka ina majina gani?, mbele yangu hapa ninayo maneno na hadith ya Imam Ali Ibn Abu Twalib (a.s), Ali Ibn Abutwalib (a.s) anajibu swali kutoka kwa mtu wa Shamu na anamwabia hivi kwanini makka imeitwa Ummul Quraa (Mama wa Vijiji),
Qur’an imeita Makka Ummul Quraa (mama wa Vijiji), huyu mtu anamuuliza Imam Ali Ibn Abutwalib ni kwani Makka imeitwa Umul Quraa? Imam Ali Ibn Abutwalib anajibu anasemaje anasema ni kwasababu ardhi imetabaazwa ,imetawanywa chini ya ardhi ya Makka.
Hii ardhi mwenyezimungu(swt) ameitawanya , mwenyezimungu amelizungumza hili katika qur’an, aya tofauti “Na ninaapa kwa ardhi na Yule alieitawanya” kwa ibara nyingine adhi ilikuwa ni donge,MwenyeziMungu(swt) akaitawanya akapasua Mito,bahari ,maziwa, milima na mabonde. Qur’an imelizungumza hili zaidi ya miaka 1400 iliyopita,
Kwaivyo kwa kuwa ardhi imetawanywa chini ya makka ndio likafanya mji wa makka uitwe Ummul Quraa (Mama wa Vijiji) kwa sababu ni mama wa miji yote,ni mama wa vijiji vyote na ndio katikati ya nchi zote.
Imam ali (a.s) anasema kunatofauti gani ya Makka na Bakka? Iko wapi makka na bakka, makka ni ile kalafu,ni ile kandokando ya haraam huwenda mtu ukatatizika kwamba mbona qur’an mara inasema Bakka, wakatimwingine inasema Makka mbona inatuchanganya Qur’an , wakati mwingine inaita Umul quraa mbona hatuielewi.
Na leo dunia watu wamesumbuka na watasumbuka, kwanini, kwasababu Yule anaeijua qur’an watu wamemuacha na siku zote na jamii yoyote ikimkamata huyu anaeijua quran na tafsiri ya quran lazima inyoke,lazima ifanikiwe.
Sasa ametueleza ali kwanini imeitwa Bakka na Umul quraa amesema Makka ni kandokando ya haram na Baka ni pale ilipo al-kaaba,kwanini imeitwa Maka kwa sababu mwenyezimungu(swt) hii ardhi ilikuwa donge, mungu akaitawanya kutoka chini ya makka. Na ndio katikakati na ndio wanapoelekea waislam wote katika swala zao, katika dua zao hata wanaposoma Qur’an.
Na huyu kiongozi atakaeleta amani duniani na maelewano duniani na kusikilizana na kupendana na dunia yote kuwa ni mahala pa maelewano chini ya bendera ya Lailaha ilallah, Muhammadun Rasulullah, mtu huyu kudhihiri kwake itakuwa siku ya ijumaa.Faraja, kheri,neema,ushindi utapatikana kwa hiyo siku atakapo dhihiri mahala hapo ni makka,atakapodhiri hapo watu watakwenda kwa magoti kumtii(kumpa baiya) Imam Mahd (a.s).
Sasa kwanini imeitwa Bakka kwa sababu Makka imewaliza majabari watu wenye kibri, watu wenye madhambi, watu wenye makosa , ukijifanya unakibri na ukaenda makka na Ukataka kuishambulia basi utarudu unalia na ndivyo ilivyotokea kwa mfalme Abraha wakati alipolituma jeshi lake kwenda kuivunja Al-kaaba.
Mmoja wa Viongozi Wakuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala
Abulmutwalib ndio muhusika wa makka akaenda kwa mfalme na akamwambia mfalme wanajeshi wako walipokuja walichukua mbuzi zangu ,hivyo naomba mbuzi zangu uzirudishe, mfalme akashangaa, akasema badala ya kuniomba nisivunje Al-kaaba unaniomba mbuzi, Abdulmutwalib akasema ile nyumba inamwenyewe, aliporudi Abraha akatuma jeshi, jeshi linaongozwa na Tembo.
Abdulmutwalib akawambia watu wa makka kimbieni milimani jeshi linakuja, wakakimbia, kisha akaenda kukamata kamba ya Al-kaaba akamwambia mungu (swt) nyumba hii ni nyumba yako ilinde nyumba yako inakuja kushambuliwa na kuvunjwa leo.
Akaacha nae akaondoka kwenda kujificha, kilichotokea mwenyezimungu (swt) anamajeshi mengi.Mungu anamajeshi kila mahala ya ardhi na mbinguni, Abraha anakuja kuvunja al-kaaba anafika hatua chache tu, Allah (swt) anawapeleka ndege wamekamata vidongo kwenye midomo yao ,vidogo vile vilikuwa na risasi wakaviachia vidongo ikawa kidongo kikikupata kwenye kichwa kinatokea chini,mwenyezimungu(swt) anasema  wakabadilika wale watu na wakasambaratika wakawa kama vile majani yaliyotobolewa tobolewa na wadudu.
Na akabakia mmoja kaenda kutoa habari, habari hizi zikasambaa dunia nzima ya warabu watu wakazidi kuiogopa Makka ,ni mahala pasipo pa kawaida na ni mahala tunasoma kila siku ndani ya Qur’an takatifu ,inshaallah mwenyeimungu(swt) atupatie nguvu tukafanye haji hiyo makka takatifu.
“Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo watenda wale wenye tembo?, Kwani hakujaalia vitimbi vyao kuharibika?, Na akawapelekea ndege makundi kwa makundi, Wakiwatupia mawe ya udongo wa Motoni, Akawafanya kama majani yaliyo liwa! , Surat A-fiil.
Sasa yoyote anaecheza na makka adui hana mwisho mzuri atasambaratika , yoyote anacheza na makka akaifanya maka  sio mahala pa amani akaifanya makka ni ardhi ya ufisadi na kuwapiga watu wasiokuwa na hatia   ajue yakwamba atalia siku moja na siku si nyingi atalia.
Kwanini makka imeitwa bakka ni kwasababu maka inawaliza au iliwaliza au inatabia ya kuwaliza, kuliza macho ya wale wenyekujifanya wakubwa na wenye madhambi.ukileta madhambi yako pale makka utasambaratishwa , ukiifanya maka haiku katika amani, jua hauna mwisho mzuri.
Bakka ni pale mahala ilipo al-kaaba na hakika makka ni haraam,mwenyekuiingia basi yupo katika amani, makka ni pale harram ambapo ni masafa makubwa , al-kaaba ni sehemu ndogo tu,lakini mahala panapoitwa harram ni mahala papana mmno. Mtu kama amefanya matatizo yake anataka kuuwawa akiingia pale yupo katika amani, mnyama anafukuzwa huko anataka kuuwawa akiingia pale yupo katika amani,njiwa wa pale huruhusiwi kumgusa
Ninawaambia waislam kumbe Dini yao sio imeweka miezi Fulani minne ni miezi ambayo huruhusiwi watu kupigana na kumwaga damu, hapana bali uislam umeweka ardhi maalum ambayo ardhi hiyo aina yoyote ya kiumbe haruhusiwi kuuwawa na kumwaga damu yake.
Uislam wa kuuwana unapatikana wapi?Uislamwa kuchinjana unapatikana wapi?,kumbe uislam sio umetaja miezi tu yakuwa katika amani, hapana bali Uislam umetaja sehemu, sehemu hiyo hatadamu ya Kunguni ni hairuhusiwi kumwagwa, hata mbu huruhusiwi kumuua, bali unatakiwa kumuondoa kwa heshima na adabu na ukimuua unatakiwa uchinje Kondoo mzima ya Kafara.Itaendelea...

No comments: