Tuesday, September 8, 2015

Yajue Maana ya Majina ya Makka Katika Qur'an na Sunna-Sheikh Hemed Jalala



Mmoja wa Viongozi Wakuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala

Watu wengi hukariri ya kwamba   maka yote ni haraam, maka yote ni ardhi takatifu yenye sheria na taratibu zile za kifiqih ambazo zinaelezwa yakwamba katika ardhi ile ni haram(hairuhusiwi) kukata miti,ni haram kumuua mnyama, ni haram(hairuhsiwi) kumwaga damu, sasa hayo ni haram kufanywa sehemu inayoitwa Haram alafu kuna Makka.
Sasa nukta yetu ya kwanza ya leo ambayo tutaizungumza Haram tutazungumzia majina ya makka, tutaanza kwanza na Qur’an takatifu, kitabu ambacho hakina shaka ndani yake ambacho ni muongozo kwa wenye kumcha Allah (swt)
Kiomgozi Mkuu wa Waislam Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala amesema kuwa Katika kuzungumzia majina ya makka napenda tuisome Suratul Al-Imraan 96, Hakika Nyumba ya kwanza walio wekewa watu kwa ibada ni ile iliyoko Bakka, iliyo barikiwa na yenye uwongofu kwa walimwengu wote” katika ayah hii mungu ameuita mji wa maka kwa jina la Bakka.
Nifaghari kubwa kwamba mungu kuweka nyumba ya kwanza iliyojengwa hapa ardhini na ikawekwa kwa ajili ya kumuabudu allah(swt) iliwekwa katika bonde takatifu la bakka, sehemu na mahala ambapo leo waislam duniani kote wanaposwali wanaelekea Makka,
ambapo allah(swt) amepaita katika Al-Imraan  ardhi ya bakka, na ndio ardhi ambayo ibada takatifu na ibada kubwa mmno na moja katika nguzo nyetu za Uislam ambayo ni Hijja inafanyika katika arhi ya bakka
Kwa hivyo aya imetudhibitishia kwamba moja ya majina ya mji takaifu wa maka ni Bakka  na ndio nchi ya kwanza na ndio msikiti wa kwanza uliowekwa duniani kwa ajili ya kumuabudu allah (swt), ama ni nani mtu wa kwanza aliouweka msikiti wa Makka hiyo ni darsa tutakalokuja kuangalia mbele ni nani alie ijenga, Je Ismail (a.s) na Ibrahim (a.s) wao ndio wakwanza walioijenga al-kaaba iliyoko katika mji wa Bakka, hizo nukta tutakuja kuzielezea hapo baadae.
Tunasoma tena suratul An-ng’am 92” Na hiki ni Kitabu tulicho kiteremsha, kilicho barikiwa, chenye kuhakikisha yaliyo tangulia, na ili uuwonye Mama wa Miji na walio pembezoni mwake. Na wenye kuamini Akhera wanakiamini hichi, nao wanazihifadhi Sala zao”
 Vile vile unaweza kusoma suratul Shuraa aya 7 “Na hiki ni kitabu tulicho kiteremsha  kilicho barikiwa  kinachosadikisha yale yaliyokuwa mbele zako, yaliokuwa mbele yake na kitabu hiki ambacho ni Qur’an ni kwaajili ya kuwahofisha watu wanaokaa kwenye mji unaoitwa Ummul Quran a wale wanaoishi kandokando ya Ummul Quraa wale walioamini akhera wanaiamini na waojuu ya swala zao ni wenye kuzichunga”
Aya inazungumzia nini? Aya hii inatidhibitishia  na kutueleza ya kwamba moja  katika majina ya mji mtakatifu wa makka ambapo mahujaji siku chache zijazo watashuka na kuporomoka katika mji huo, mwenyezimungu(swt) ameuita vilevile ndani ya qur’an Ummul Quraa( mama wa Vijiji).
Kama kuna kijiji kinafaghari kubwa kinaweza kukusanya kila aina ya faghari basi kijiji cha Makka, kijiji kilichopo katika bonde takatifu la Bakka,kijiji hicho ni kijiji ambacho hakina mfano wake, kijiji hicho ni Ummul Quraa(Mama wa Vijiji).
Suratul Fatihi 24, “Na Yeye ndiye aliyeizuia mikono yao kwenu, na mikono yenu kwao, katika bonde la Makka baada ya kukupeni Ushindi juu yao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona myatendayo”
Aya inazungumza mwenyezimungu vipi amewanusuru waislam na kuwasaidia waislam na kuwaunga mkono waislam, lakini hayo yametokea wapi? Yametokea katikati ya mji wa makka.
Aya hizi tatu zinatuwekea barabara ya kwamba Makka inamajina mengi yaliyoitwa ndani ya Qur’an katika majina hayo ni Bakka,Makka na Ummul Quraa ( Mama wa Vijiji), aya hizi zinamaelezo marefu lakini kwa kuwa nipo katika maelekezo na katika darsa ya kubainisha majina ya makka sitoingia kuzisherehesha aya hizo kwa kirefu.
Napenda tuingie katika Sunna katika Riwayat tuziulize riwayat makka ina majina gani?, mbele yangu hapa ninayo maneno na hadith ya Imam Ali Ibn Abu Twalib (a.s), Ali Ibn Abutwalib (a.s) anajibu swali kutoka kwa mtu wa Shamu na anamwabia hivi kwanini makka imeitwa Ummul Quraa (Mama wa Vijiji),
Qur’an imeita Makka Ummul Quraa (mama wa Vijiji), huyu mtu anamuuliza Imam Ali Ibn Abutwalib ni kwani Makka imeitwa Umul Quraa? Imam Ali Ibn Abutwalib anajibu anasemaje anasema ni kwasababu ardhi imetabaazwa ,imetawanywa chini ya ardhi ya Makka.
Hii ardhi mwenyezimungu(swt) ameitawanya , mwenyezimungu amelizungumza hili katika qur’an, aya tofauti “Na ninaapa kwa ardhi na Yule alieitawanya” kwa ibara nyingine adhi ilikuwa ni donge,MwenyeziMungu(swt) akaitawanya akapasua Mito,bahari ,maziwa, milima na mabonde. Qur’an imelizungumza hili zaidi ya miaka 1400 iliyopita,
Kwaivyo kwa kuwa ardhi imetawanywa chini ya makka ndio likafanya mji wa makka uitwe Ummul Quraa (Mama wa Vijiji) kwa sababu ni mama wa miji yote,ni mama wa vijiji vyote na ndio katikati ya nchi zote.
Imam ali (a.s) anasema kunatofauti gani ya Makka na Bakka? Iko wapi makka na bakka, makka ni ile kalafu,ni ile kandokando ya haraam huwenda mtu ukatatizika kwamba mbona qur’an mara inasema Bakka, wakatimwingine inasema Makka mbona inatuchanganya Qur’an , wakati mwingine inaita Umul quraa mbona hatuielewi. Inaendelea Ukurasa Ujao

No comments: