Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala akiongea katika Maulidi hiyo, Dar es salaam. |
Kiongozi
Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala
amewataka Watanzania kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w)
kwani Maulid inafundisha kupinga Dhulma, Ugaidi na Umuhimu wa Amani.
“Moja ya
funzo ilikuwa ni kupambana na dhulma, na ndio maana Mtume akasema Msaidie ndugu
yako akiwa amedhulumu au akiwa amedhulumiwa, kubwa ni kupinga vita dhulma,
dunia leo hakuna shaka kuwa imegubikwa na dhulma katika Nyanja zote, ili
kuiondoa dhulma tunaihitajia vikao hivi vya Maulid ya Mtume Muhammad (s.a.w.w).”
amesema Sheikh Jalala
Sheikh Jalala amesema hayo leo katika Sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) imeyofanyika katika ukumbi wa Urban Rose Hotel, Jijini Dar es salaam.
Aidha Sheikh
Jalala amesema kuwa tunapokuwa tunakumbuka kuzaliwa Mtume Muhamad (s.a.w.w)tunasoma
mafundisho yake yalikuwa yanapinga aina zote za Ubaguzi.
“Dunia leo
imegubikwa na kuwafanya watu kuwa wanyonge, kuwagawanya watu katika matabaka,
ubaguzi bado upo hata kama ni wa kifikra bado unatawala dunia, Mtume Muhammad
(s.a.w.w) alipambana na Ubaguzi.”
“Mtume
Muhammad (s.a.w.w) alikuja kuwafundisha watu kuwa watu wote wako sawa, leo
dunia imekuja kuwagawanya watu, watu wa ulimwengu wa tatu, ulimwengu wa pili,
watu wenye haki ya kumiliki, watu wasiokuwa na haki ya kumiliki, watu
wanaofaidika na rasilimali walizonazo, watu wasiofaidika na rasilimali
walionazo” amesema Sheikh Jalala
Sheikh
Jalala amesema kuwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika mafunzo aliyoyafunza ni
funzo la amani, kwamba Mungu tunaemuabudu ni Mungu wa Amani kwa mungu siku zote
inatoka Amani, leo tunaona kwa pamoja mashariki ya kati na dunia kwa ujumla
imegubikwa na kitu kinachoitwa ugaidi, imegubikwa na ukatili kupita kiasi,
imegubikwa ni kuchinjana ni mateso hujawahi kuyaona hata kuyasikia katika
maisha yako.
“Niseme kwa
masikitiko makubwa kauli ya Raisi wa Marekani Donard Trump yakuufanya Mji
mtakatifu wa Palestina Masjid Aqswa mji mtakatifu wa Jerusalem, ambapo ndani yake
kuna Qibla ya Waislamu kuufanya mji mkuu badala ya Teleavivi hiki ni kinyume na
ubinadamu na nikinyume na tofauti katika kuenzi Amani, kupenda watu kukaa
vizuri, wakae kwa salama”.Amesisitiza Sheikh Jalala
Kadhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam amabae ni Imam Mkuu wa Msikiti wa Manyema Sheikh Hamid Jongo akiongea na Waandishi. |
Kwa Upande
wake Kadhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambae pia ni Imam Mkuu wa Masjid
Manyema Sheikh Hamid Jongo amewataka watanzania kulinda na kuienzi amani,
utulivu na mshikanamo tulionao waislamu na wakristo hapa nchini.
“Natoa wito
kwa watanzania hivi tulivyo amani, ushirikiano na utulivu tuupiganie kwani hii
ndio jihadi yetu kuhakikisha vitu hivi vinadumu amani, utulivu na mshikamano na
kuishi kwa kuridhiana baina ya watu wa dini zote” amesisitiza Sheikh Jongo.
No comments:
Post a Comment