Friday, October 14, 2016

SHEIKH ALHAD MUSSA: WATANZANIA FATENI MAFUNDISHO NA MATENDO YA IMAN HUSSEIN (A.S) KWA KUTENDA HAKI NA KUKATAA DHULUMA

Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Alhad Mussa Salum wa pili kutoka Kushoto akiwa katika matembezi ya Amani yaliyofanyika Jijini Dar es salaam yaliyoandaliwa na waumini wa Khoja Shia Ithanasheriya Tanzania ikiwa ni Ishara ya kumkumbuka Mjukuu wa mtume Muhamad ambaye ni Imam Hussein.

Akizungumza na wanahabari wakati wa maandamano hayo ya amani Sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es salaam amewataka watanzania kufwata Nyayo za Iman Hussein ambaye alipenda haki na kukataaa dhuluma miongoni mwa Jamii pamoja na kutunza amani ilipo nchini Mwetu.

Aidha amezitaka Taasisi za kidini nchini kujenga Umoja na mshikamano miongoni mwao bila kujali imani na itikadi za dini zao ili kujenga Taifa lenye umoja na mshikamano na upendo kwa wote.
 
 Waumini wa Dini ya kiislam Kutoka jumuiya ya kiislam Khoja Shia Ithnasheriya Tanzania wakiwa katika maandamano ya amani Jijini Dar es salaam  ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya Kifo cha Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w),ambaye ni Imam Hussein (a.s),maandamano ambayo yameanzia katika msikiti wa Kablastan hadi msikiti wa Khoja Shia Ithnasheriya jijini dar es salaam
 
 Kiongozi mkuu wa waislam dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akizungumza na wanahabari wakati wa maandamano hayo Jijini Dar es salaam ambapo pamoja na mambo mengine Sheikh Jalala amendelea kusisitiza watanzania kutunza  amani na umoja uliopo pamoja na kufwata yale ambayo Imam Hussein alikuwa akiyatenda wakati uhai wake ikiwemo kupinga ukandamizaji, dhuluma katika jamii na kujenga umoja na mshikamano katika jamii.

No comments: