Naibu Kiongozi Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Muhammad Abdi akizungumza na wanahabari Masjid Ghadir, Kigogo POST Dar es salaam |
Naibu Kiongozi Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Muhamad Abdi ameitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutenge sehemu maalumu au kiwango maalumu kwa ajili ya watoto yatima ambapo leo hii tunao wengi katika maeneo yetu.
"Wito wetu kwa watu wenye uwezo na hususan Serikali yetu itenge sehemu maalumu au kiwango maalumu kwa ajili ya watoto yatima ambapo leo hii tunao wengi katika maeneo yetu." Sheikh Abdi
Sheikh Abdi amesema hayo katika program ya mayatima yaliyoandaliwa kwa kuadhimisha Kifo cha Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), ambae ni Imam Hussein (a.s), Jana Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam.
"Ni kazi nzuri ya kumlea yatima ambayo faida yake inapatikana hapa duniani na kesho akhera, faida ya hapa duniani utakuwa umeweza kumuondolea mtoto huyo yatima mashaka, dhiki na utakuwa umepunguza rundikano la watoto amabo hawana malezi, makazi na chakula" amesema sheikh Abdi
Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika maneno yake mazuri anasema "mimi mtu ambae anamlea yatima, mtu ambae anamtazama yatima, mtu ambae anampa matumzo yatima tutakuwa pamoja katika pepo"
Imam Hussein (a.s) Babu yake ni Mtume Muhammad (s.a.w.w), bibi yake ni Mke wa Mtume Bi Khadija (a.s), Baba yake ni Imam Ali (a.s) na Mama yake ni Mtoto wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) Bi Fatuma (a.s).
Hatahivyo jambo la kutomjali Yatima ni jambo halipendi Mungu " je unamjua yule mtu ambae anakadhibisha dini na malipo na anaemsukuma yatima ni yule ambae anamnyanyasa yatima, watoto yatima katika jamii yetu wapo wengi lakini, walio wengi hawapati mahitaji wanayohistahiki.
"Hakuna fadhilia kubwa kama kumtizama mtoto yatima, kumsaidia anapokuwa na matatizo, kumlea vizuri na hii na hii ni moja katika kazi Mwenyezimungu (swt) anapenda na ni moja ya kazi zetu katika moja ya kituo chetu cha Imam Swadiq tawi la Sungwi" Sheikh Abdi
Baadhi ya Watoto yatima waliohudhuria Masjid Ghadir, kwa kuadhimisha Kifo cha Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), Imama Hussein (a.s) |
No comments:
Post a Comment