Sheikh Abdullatwif Swalehe akito hotuba juu ya siku ya Huzuni kwa Kubomolewa Makaburi Matukufu
Sheikh Abdullawif Swalehe aliuliza kuwa kama Fatwa
ya kupomoa Makaburi ni Sahihi, ni kwanini makaburi ya khalifa wa kwanza Abubakar
na wapili Omar hayajabomlewa ambayo yamejengwa ndani ya msikiti?
Amesema kitendo cha Utawala wa Kiwahhabi (Answar
Sunna) cha kutoa fatwa za kuhalalisha makaburi na sehemu tukufu za Mkumbusho ya
Waislam kupomolewa , ni kitendo ambacho kinachopingana na Qur’an tukufu ya
Allah (swt).
Hayo aliyasema Jana katika Maadhimisho ya Siku ya
Huzuni (Majonzi) yaliyofanyika Msikitini Ghadir Kigogo-Post, Dar es salaam
ambayo huwa yanafanyika kila mwaka katika tarehe kama hii ya Shawwal 8 1344.
“Jamii yoyote huwa inatunza na kudumisha athari za
matukio muhimu ili watu wengine waweze kuzitambua kama matukio yalifanywa na
Mitume.Maimam, Makhalifa na Waja wema wa Allah (swt) alisema Sheikh Swalehe.
|
No comments:
Post a Comment