Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Kikwete anatarajia kuwa
mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa
itakayofanyika Julai 25, 2015 Katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar
es salaam.
Akizungumza
mara baada ya kukamilika kwa maandalizi ya maadhimisho hayo leo jijini
Dar es salaam,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki amesema
maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika jijini Dar es salaam kuwakumbuka na
kuwaenzi mashujaa waliojitoa muhanga kupigania uhuru na ukombozi wa
Taifa la Tanzania,kulinda na kudumisha amani na utulivu wa nchi.
Amesema
Maadhimisho hayo yatapambwa na Gwaride la Kumbukumbu litakaloandaliwa
na vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),Polisi ,Magereza na
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Aidha,
amesema kutakuwa na Mizinga salama itakayopigwa, uwekaji wa silaha za
asili na maua kwenye mnara wa kumbukumbu, Kutakuwa na sala na Dua
kutoka kwa viongozi wa
Bw.
Sadiki amefafanua kuwa shughuli zote katika viwanja vya Mnazi Mmoja
zitaanza saa mbili Asubuhi na kumalizika saa sita mchana ambapo wananchi
watakaohudhuria kumbukumbu hiyo watapata fursa ya kushuhudia matukio
yatakayokuwa yananendelea uwanjani hapo kupitia Luninga kubwa
zitakazokuwepo katika maeneo yote muhimu ya uwanja.
Ameongeza
kuwa siku hiyo baadhi ya barabara katika jiji la Dar es Salaam zikiwemo
Lumumba ,Uhuru na Bibi Titi zitafungwa kwa muda ili kuhakikisha
usalama wa watumiaji wa barabara hizo watakaohudhuria maadhimisho hayo .
Katika
hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ametoa ufafanuzi kuhusu
changamoto zinazoendelea kujitokeza za kusuasua kwa zoezi uandikishaji
wa wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura katika mfumo wa BVR
jijini Dar es Salaam.
Amesema
kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kushirikiana na Wakurugenzi wa
Manispaa za jiji la Dar es Salaam wanaendelea kushughulikia matatizo
mbalimbali yaliyojitokeza katika siku ya kwanza na ya pili katika baadhi
ya vituo hususani baadhi ya mashine za BVR kushindwa kufanya kazi
vizuri.
Akizungumzia
baadhi ya malalamiko yanayotolewa na wananchi hasa tatizo la uchelewaji
wa waandikishaji kufika katika vituo walivyopangiwa kwa wakati amesema
kuwa Serikali ianaendelea kuchukua hatua ili kukomesha tabia hiyo.
Amewaagiza
Wakurugenzi wa Manispaa zote za jiji la Dar es Salaam kuwachukulia
hatua watumishi hao wazembe kwa kuwafuta kazi ili kuepusha madhara na
vurugu zinazoweza kuepukika na uongeza kuwa kazi ya uandikishaji
wananchi inatakiwa kuanza saa 2 asubuhi mpaka saa 12 jioni kila siku kwa
tarehe zilizopangwa.
Kuhusu
taarifa za uwepo wa baadhi ya watendaji kuwaingiza waandikishaji
wasiohusika kusimamia zoezi hilo Mkuu wa Mkoa huo amewataka watendaji
hao kuacha mara moja tabia hiyo ili kuepuka kuvuruga zoezi hilo na
kwamba hatua kali za kisheria zitachuliwa dhidi yao.
Pia
amevitaka Vyama vya siasa kuacha kutumia mwanya huo kuweka bendera au
kuvaa mavazi yanayoashiria kampeni za siasa ili kuepusha vurugu.
No comments:
Post a Comment