Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametofautina mtazamo kuhusu ushoga na
ndoa za jinsia moja na mgeni wake ambaye ni Rais wa Marekani, Barack
Obama mbele ya waandishi wa habari.
Akiongea mbele ya idadi kubwa ya waandishi wa habari katika eneo la
Ikulu ya Kenya, Rais Obama alipinga kwa nguvu ubaguzi dhidi ya watu
wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, lakini Uhuru Kenyatta alikuwa
ngangari na kumueleza kuwa utamaduni huo hauna nafasi nchini Kenya.
Rais Kenyatta alifafanua kuwa suala la ushoga sio suala muhimu nchini
humo na kwamba nchi hiyo inahitaji kujikita katika maeneo mengine
ambayo ndiyo maisha ya kila siku ya wananchi.
Obama aliingia nchini Kenya Julai 24 usiku na kupata mapokezi ya
kihistoria katika nchi hiyo inayomchukulia kama mtoto wa nyumbani
aliyerudi na taji la ukuu wa nchi kubwa yenye nguvu zaidi duniani.
No comments:
Post a Comment