Waislamu wanaoishi Marekani wameandama mbele ya ubalozi wa Saudi Arabia
mjini Washington wakilalamikia jinai za nch hiyo na hatua ya nchi hiyo
ya kuunga mkono ugaidi.
Shirika la habari la Tasnim limeripoti kutoka
Washington kuwa, maelfu ya Waislamu wanaoishi katika maeneo ya kaskazini
na katikati mwa Marekani jana walikusanyika kwenye maidani ya Watergate
mjini Washington na kisha kuandamana hadi mbele ya ubalozi wa Saudia na
kupiga shaari dhidi ya serikali ya Riyadh.
Wafanya maandamano hao
walikuwa wakipiga nara na shaari kama
"utawala wa Aal Saud si tu si
mwakilishi wa Uislamu, bali ni muungaji mkono wa kundi la kigaidi la
Daesh, machafuko na misimamo ya kufurutu ada.” Katika maandamano hayo,
Hujattul Islam wal Muslimin Sheikh Abduljalil Imam wa msikiti wa
Jaafariya huko Maryland Marekani ametoa hotuba na kulaani jinai za Saudi
Arabia.
Sheikh Abduljalil ameendelea kuhutubia kwa kusema wamekusanyika
ili kuwaambia walimwengu kwamba iwapo wanatafuta chanzo cha magaidi
basi wanapasa kukipata ndani ya utawala wa Aal Saud.
Amesema chimbuko la
ugaidi katika eneo la Mashariki ya Kati, huko Iraq na Syria ni utawala
huo wa Aal Saud.
Chanzo Irib.
No comments:
Post a Comment