Sunday, June 28, 2015

Sheikh Waziri Nyelo afanya Ziara Makaburini

 Sheikh Waziri Nyello aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislam wa Madhehebu ya Shia Ithna Ashariyyah Tanzania, amewaongoza wana kijiji wa Nyasa kwenye kisomo maalumu kwa ajili ya kuwa kumbuka Marehemu na waasisi wa kijiji hicho.

Tukio hilo  limetoa katika Mkoa wa Tanga wilaya ya Lushoto , kumbukumbu hii huwa inafanyika kwa kila mwaka ifikapo Ramadhan ya 9 ikiwa ni sehemu ya kuunganisha umoja na mshikamano baina ya Waislamu. 

Ziara ya makaburi ni jambo lililoruhusiwa kisheria, ni jambo lenye faida kwa walio hai ili wawaidhike na iwakumbushe na akhera ajue mwenye kuzuru kaburi kuwa hapo alipo nduguye naye atakuwamo siku moja. Hali kadhalika faida nyingine ni kuwaombea nduguze waislamu na huyo maiti wake.

Inafaa kwa Mwislamu kila wiki kwa uchache hasa siku AIhamisi awakumbuke wafu wake kwa kufika kwenye makaburi yao, hii ni Sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w) akiwaamrisha Masahaba wake kuzuru makaburi.

Licha ya kuwepo wapokezi wa hadithi kuhusu jambo hilo kutokana na wanachuoni, wa Ki-Shia vile vile wamepokea hadith hizo wanachuoni wa Ki-Sunni nao ni: Bwana Muslim katika Saheeh yake, na Bwana Bayhaki katika 'Sunan' yake na pia Bwana Ahmad Bin Hambal, Bwana Abudaud, Bwana Tirmizi, Bwana Nasaina Bwana Baghawi.

Ni sunna unapofika kwenye kaburi uelekee Qibla, weka mkono kwenye hilo kaburi na soma mara saba (7) sura ya Innaa Anzalnahu (5:97) na pia bora usome sura ya AL-FAATlHA (S:1) na sura ya AL-FALAQ (5:113) na WAN-NASI (S:114) na sura ya QUL-HUWL-LAAHU (S:112) na Ayatul-Kursi kila moja mara tatu.



No comments: