Askari
wa Jeshi la Polisi Said Kombo anayefanyia kazi katika kituo cha Polisi
Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba anashikiliwa na jeshi la Polisi
kwa tuhuma za kumuuwa mama mzazi kwa kumchoma kitu chenye ncha kali .
Askari huyo ambaye anadaiwa kuwa ni mgonjwa wa akili ametekeleza kitendo hicho jana majira ya saa tano za asubuhi ambapo inadaiwa kuwa alimchoma mama mzazi Mwanaisha Haroun Hamad .
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi daktari wa zamu katika Hospitali ya Micheweni Mkubwa Habib amekiri kupokea mwili wa marehemu huyo ambaye alikuwa amejeruhiwa sehemu mbali mbali za mwili wake .
Amefahamisha kwamba marehemu huyo alikuwa amepata majeraha sehemu za mgongoni , mikononi na kifuani na kuongeza kifo chake kimetokana na kutokwa damu nyingi .
“Ni kweli nimepokea majeruhi ambaye alikuwa amejeruhiwa sehemu mbali mbali za mwili wake na kitu chenye ncha kali , na alipofikishwa hapa alikuwa hana tana fahamu ”alifahamisha .
“Baada ya kuufanyia uchunguzi mwili wake nilibaini kuwepo na majeraha sehemu za mgongoni , mikononi pamoja na kifuani ambapo alikuwa anatoka damu katika mwili wake ”aliongeza
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa walisikia kelele na walipofika wakimkuta marehemu akiwa anatoka damu sehemu za mwili na walichukua hauta za kumpeleka hospitali kabla ya kutoa taarifa kwa jeshi la Polisi .
“Mimi niliskia kelele na nilipofika nilimkuta anatoka damu nyingi na tuliamua kumpeleka hospitali kwanza kupata matibabu na baadaye tulipeleka taarifa kwa jeshsi la Polisi ”alieleza mmoja wa wananchi akiwa hospitalini hapo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Kamishina Msaidizi Shekhan Mohammed Shekhan amesema kuwa mtuhumiwa huyo kwa sasa anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa hatua za upelelezi.
Alieleza kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo linendelea kumuhojiwa mtuhumiwa huyo kwa ajili ya kukamilisha taratibu na badae kumfikisha mahakamani kwa taratibu za kisheria zaidi dhidi yake.
“Baada ya tukio kutokea Askari wa Jeshi la Polisi walimkamata mtuhumiwa na kwa sasa tunaendelea kumhoji na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinamkabili upelelezi utakapo kamilika ”alieleza Kamanda Shekhan .
Hata hivyo kamanda Shekhan amewataka wananchi wanaosihi na wagonjwa wa akili kuwapeleka Hospitali kwa ajili ya kupata matibabu na kuacha kuwafungia ndani ili kuwalinda na madhara yanayoweza kuwapata
Chanzo Habari24.net
No comments:
Post a Comment