Obama, Clinton washerehekea, Republican walaani
Rais Barack Obama, ambaye ni rais wa kwanza alieko madarakani kuunga
mkono waziwazi ndoa za jinsia moja, alisifu hukumu hiyo, akisema kwenye
mtandao wake wa twitter kuwa siku ya leo ni hatua muhimu katika safari
ya kuhakikisha usawa kwa watu wote.
Naye Hillary Clinton, mgombea anaepewa nafasi kubwa kupitishwa na chama
Demokratic kuwania urais mwaka 2016, aliandika kwenye mtandao wake wa
twitter kuwa "Najivunia kusherehekea ushindi wa usawa wa ndoa." Hadi
mwaka 2013, Clinton alisema alikuwa anapinga ndoa za jinsia moja, lakini
alibadili mtazamamo wake tangu wakati huo.
Rais Barack Obama ameitaja hukumu hiyo kuwa ni ushindi wa usawa nchini Marekani.
Mgombea wa chama cha Republican Mike Hackabee alisema, uamuzi huu wa
udanganyifu ni uababe wa mahakama unaokwenda kinyume na katiba." Mgombea
mwingine wa Republican Jeb Bush aliongeza kuwa, " nikiongozwa na imani
yangum naamini katika ndoa za asili. Naamini mahakama kuu ilipaswa
kuyaruhusu majimbo yafanye uamuzi huu.
Ndoa za jinsia moja zilikuwa zinaruhusiwa katika majimbo 36 ya Marekani
pamja na Washington DC. Katika jimbo la 37 la Alabama, mahakama iliondoa
marufuku dhidi ya ndoa za jinsia moja, lakini mahakama ya rufaa
iliwazuwia maafisa wa serikali kutoa leseni kwa wapenzi wa jinsia moja.
Wapinzani wa ndoa hizo wanasema uhalali wake unapaswa kuamuliwa na
majimbo yenyewe, na wengine wanasema kuruhusiwa kwa ndoa hizo ni dharau
kwa ndoa ya asili kati ya mwanamume na mwanamke, na kwamba Biblia
inalaani mahusiano ya jinsia moja.
Hisia juu ya hilo zilikuwa juu wakati wa mjadala mahakamani mwezi April
katika kesi hiyo, pale mwandamanaji alipowapigia kelele majaji na
kuwambia wataozea jahanam ikiwa watapitisha hukumu kuunga mkono ndoa za
jinsia moja.Chanzo BBC Swahili
No comments:
Post a Comment