Monday, September 28, 2015

Ban: Mgogoro wa Yemen hauwezi kutatuliwa kwa silaha

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa mgogoro wa Yemen hauwezi kutatuliwa kwa njia za kijeshi.
Ban Ki-moon ameyasema hayo leo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 70 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York. 
Amesema kuwa kwa sasa inaoneka kuwa, kupata fedha kwa ajili ya kuua watu katika nchi zao ni rahisi zaidi kuliko kupata fedha kwa ajili ya kuwalinda watu. Ban Ki-moon amesema kuwa mashaka na matatizo ya mwanadamu wa leo hayana kifani na kwamba kizazi kipichopita cha mwanadamu hakikukumbana na mashaka makubwa kama haya.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa kwa sasa watu milioni 100 wanahitaji msaada na wengine milioni 60 wamelazimika kukimbia makazi yao. Amesisitiza kuwa kwa sasa kuna udharura wa kupatikana utatuzi wa kudumu wa migogoro wa dunia.
Amesifu jitihada zinazofanywa na Ulaya kuwasaidia wakimbizi na akatoa wito wa kutafutwa njia zenye taathira zaidi katika uwanja huo.
Vilevile katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewataka wahusika wakuu katika eneo la Mashariki ya Kati kuchukua hatua za kukomesha mgogoro wa Syria.chanzo irib

No comments: