Mmoja wa viongozi wakuu wa kiroho wa
waislamu, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala
amesema maafa yaliyotokea Hijja sio mpango wa Mungu bali yamesababibshwa
na serikali ya Saudi-Arabia
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini
Dares salaam baada ya kurejea kutoka Hijja alfajiri ya leo Sheikh
Jalala amebainisha kuwa serikali ya Saudia inapaswa kukiri kuhusika na
maafa hayo kwakuwa kulikuwa na usimamizi mmbovu uliopelekea maafa hayo
Akibainisha sababu za serikali ya Saudia
kubeba mzigo wa lawama Jalala amesema kitendo cha kufunga barabara mbili
zenye ukubwa wa mita 30 zinazo elekea eneo la jamarati na kuwaacha
mahujaji kutumia barabara ndogo ndio chanzo kikubwa cha maafa ya
mahujaji wakati wakitekeleza ibada ya kumpiga mawe shetani.
Hata hivyo ameongeza kuwa licha ya eneo
kuwa na kamera kila kona lakini mahujaji waliokuwa wakipoteza maisha
kila baada ya dakika tano hawakuweza kuokolewa na hata kitengo cha
msaada wa kwanza hakikutimiza majukumu yake kikamilifu jambo ambalo
lilipelekea idadi ya vifo vingi
Aidha sheikh Jalala amesema jambo
hilo ni la kusikitisha na kwamba haitakuwa busara kulikalia kimya
kwakuwa idadi ya watu waliopoteza maisha na ambao mpaka sasa
hawajulikani walipo ni kubwa saana na kwamba serikali ya Tanzania
inapaswa kuliingilia kati kwa kuwa watu walienda maka kuhiji na sio
kupoteza maisha.
Katika ibada ya Hijja mwaka huu zaidi ya mahujaji 700 wameripotiwa kupoteza maisha katika mkanyagano tofauti na hijja zingine.
No comments:
Post a Comment