Saturday, March 21, 2015

Viongozi wa Hawzat Imam Swadiq (a.s) wamlilia Fatma (a.s) Bint ya Mtume (s.a.w.w)

Kulia ni Sheikh Muhammad Abdi Naibu wa Hawzat Imam Swadiq (a.s) Kigogo-Post Dar es salaam. Kushoto ni Sheikh Qassim Ruvakule.
Bibi Fatma (a.s) ni bint wa pekee aliyeishi katika mabinti wa bwana mtume (s.a.w.w), ni mtoto wa mwanake bora miongoni mwa wale wanawake bora wanne waliochaguliwa na Allah ambaye ni Khadija bint Khuwailid.

Mtume wa Allah anasema “Fatima ni pande la nyama katika sehemu ya mwili wangu, atakaemridhisha ameniridhisha mimi na atakaemuudhi ameniudhi mimi”.

Kulia ni Sheikh Abdullatwif Swaleh.

Tukio la kuchomwa moto nyumba ya sayyidat fatima (a.s) na ambalo ndio lililokuwa chanzo cha kifo chake cha kishahidi."Wallah! Wewe Ali utoke nje utoe Baia Kwa Khalifa wa Mtume, kinyume chake nitawasha moto katika nyumba hii." Fatima (a.s) akasimama na akasema: Ewe Umar unanini wewe na sisi? Umar akasema: "Fungua mlango, na usipofungua mlango nitaichoma moto nyumba yenu mkiwa ndani yake" Fatima (a.s) akasema

Kushoto ni Sheikh Qassim Ruvakule pamoja na Sheikh Muhammed Abdi wakionesha huzuni kubwa kwa kifo cha Fatma (a.s) bint ya Mtume Muhammad (s.a.w.w).

"Ewe Baba yangu! Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu (s.w)! Umar akainua upanga wake uliokuwa kwenye ala yake (Scabbard) na kuuweka upande wa shingo ya Sayyidat Fatima (a.s), Fatima (a.s) akapiga tena ukelele kwa sauti ya juu kabisa akiita: 

Naibu Imam wa Msikiti wa Ghadir Kigogo-Post Sheikh Nyambwa pembeni yake akiwa na Sheikh Muhammad Abdi.

"Ewe Baba yangu". Basi Umar akaona afanyeje ili kumnyamazisha Fatima (a.s) aachane na ukelele huo wa Kumuita Baba yake Mtume (s.a.w).akawaza na kuwazua, likamjia wazo! Akaamua kunyanyua mjeredi wake na kumchapa nao Sayyidat Fatima (a.s) sehemu ya mgongo wake. Fatima (a.s) akaita kwa sauti ya juu

Hawa ni Viongozi wa Hawzat Imam Swadiq (a.s) wakionesha huzuni kubwa ya kukumbuka kifo cha Fatma (a.s) bint ya Mtume (s.a.w.w).

Hisia hizo zimetokea leo Msikitini Ghadir Kigogo-Post, Dar es salaam, katika Maadhimisho ya kukumbuka kifo cha Fatma (a.s) ambao yameandaliwa na Hawzat Imam Swadiq (a.s).

No comments: