Saturday, March 21, 2015

Hawzat Imam Swadiq (a.s) yaadhimisha kifo cha Fatma (a.s)

Mwanafunzi wa Hawzat Imam Swadiq (a.s) Rajab Majid wa  Darasa la 3, akisoma Ziara 

Mwanafunzi wa Hawzat Imam Swadiq (a.s) Baqir Asghar ,Darasa la Kwanza, akisoma Qur'an tukufu.

Mwanafunzi wa Hawzat Imam Swadiq (a.s) Hassan Omary akisoma Shairi la kuhuzunisha la juu ya Tukio la kuangukiwa Mlango Fatma Zahra (a.s).

Mwalimu wa Hawzat Imam Swadiq (a.s) Sheikh Qassim Ruvakule, amewataka Waislam Wote kuutambua Utukufu wa Fatma Zahra Bint ya Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Kumbukumbu hizi za Kukumbuka Kifo cha Fatma Zahra (a.s) zimeandaliwa na Hawzat Imam Swadiq (a.s) ambazo zimefanyika leo katika Msikiti wa Ghadir Kigogo-Post, Dar es salaam.

Bibi Fatma (a.s) ni bint wa pekee aliyeishi katika mabinti wa bwana mtume (s.a.w.w), ni mtoto wa mwanake bora miongoni mwa wale wanawake bora wanne waliochaguliwa na Allah ambaye ni Khadija bint Khuwailid.


Bibi Fatima aliuawa na wale walioshika madaraka baada ya Mtume (s.a.w.w) ambao ni Abubakar (r.a) na Omar (r.a) na alizikwa usikua bila watu kujua. 


Wanafunzi wa Hawzat Imam Swadiq (a.s) wakiongozwa na Zaynul Abidiin, wakiimba Qaswida (Nauha) ikiuliza "Nielezeni ni wapi amezikwa Fatma (a.s)


No comments: