Saturday, March 21, 2015

Sheikh.Abdi “Umuhimu wa usomaji Qur’an Nyumbani”

Naibu Mkuu wa Hawzat Imam Swadiq (a.s) akihutubu jana katika swalat Jumaa.
Naibu Imamu Sheikh Muhammed Abdi amewataka waumini wa Dini ya Kiislam kujibidisha na kujikurubisha katika Usomaji wa Qur’an.

Hayo aliyasema jana katika Hutuba ya Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Ghadir Kigogo-Post, Dar es salaam.

Sheikh.  Abdi alisema  umuhimu wa nyumba inayosomwa QUR'AN, Allah huifanya Nyumba hiyo kuwa pana na Nyepesi riziki yake pamoja , huiweka katika Ulinzi wake na chini ya Ngome yake.

Aliongeza kuwa allah (swt) huwakinga na Umasiki na Ufukara watu wake na Huwaepusha na Mabalaa na Kila aina Shari zinazosababishwa na majini pamoja na watu.

Waumini wa Dini ya Kiislam, dhehebu la Shia wakiwa msikikiti wakiomba dua baada ya kumaliza swala ya Ijumaa

Waumini wakiwa katika hali ya Utulivu mbele ya Mwenyezimngu (swt) wakijiandaa kufanya Nyurad (Tasbih) mbalimbali za baada ya swala ya Ijumaa

No comments: