Balozi na Naibu Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu
ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, uvamizi na ukaliaji
mabavu wa Wazayuni ndio tishio kubwa zaidi la usalama na amani ya dunia.
Ghulam Hussein Dehqani, amesema hayo katika kikao cha kila
mwaka cha kamati ya nne ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo
sambamba na kuashiria kuongezeka vitendo vya utumiaji mabavu vya
utawala haramu wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina amesema kuwa,
uvamizi na ukaliaji mabavu wa Wazayuni dhidi ya ardhi za Palestina ndio
tishio kubwa zaidi la amani na usalama wa dunia.
Amesema kuwa, kuna haja ya kuchukuliwa hatua za kilimwengu kwa ajili ya kukabiliana na hatua hizo za utawala dhalumu wa Israel.
Balozi na Naibu Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika
Umoja wa Mataifa sambamba na kukumbusha kushadidi vitendo vya utumiaji
mabavu na mauaji ya Israel dhidi ya wananchi madhulumi wa Palestina
pamoja na hali yao mbaya amebainisha kwamba, kuna haja ya kuongezwa
mashinikizo ya jamii ya kimataifa dhidi ya utawala huo ghasibu ili
uhitimishe vitendo na hatua zake zisizo za kisheria dhidi ya wananchi wa
Palestina.
Ghulam Hussein Dehqani amesema kuwa, mazingira mabaya ya kibinadamu
katika Ukanda wa Gaza ambayo yametokana na kuendelea mzingiro dhidi yao
na vikwazo vya kiuchumi yamepelekea hali ya eneo hilo kuchukua mkondo
mpana zaidi.
No comments:
Post a Comment