Friday, January 16, 2015

"Kitendo cha Jarida La Charlie Hebdo kumdhalilisha Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni kitendo cha Kifedhuli”.



Harakati ya hawza Imam Swadiq chini ya Uongozi wa Samahat Sheikh Hemedi Jalala inaungana na Waislamu wote duniani na Wapenzi wa Amani kokote walipo kupinga kwa Kauli thabiti hatua zozote zinazochukulia na Serikali za nchi za Magharibi na Marekani kuchochea vitendo venye lengo la kuamsha chuki na machafuko ya Kidini ulimwenguni.


Jalala alisema kitendo cha kumtusi Muhammad (s.a.w.w) ni Kashfa na Matusi ya wazi kwa Mtume wetu Kipenzi chetu Muhammad (s.a.w.w) Waislamu wote bali na wapenda Amani duniani kote. Ni kitendo kisichovumilika na hakuna Musialmu aweze kustahamili ghadhabu zake kwa kitendo hichi.

Kauli hivyo imetolewa baada tu ya Jarida linalochapisha vibonzo mjini Paris nchini Ufaransa Charlie Hebdo lilisema katika toleo lake la hapo kesho siku ya Jumatano(14/01/2015) litachapisha kibonzo cha Mtume Muhammad katika ukurasa wa mbele, akiwa na bango lenye maandishi “Je suis Charlie”, ikimaanisha “mimi ni charlie nimesamehe yote”.
Aidha alisema kuwa vitendo hivi vinafanywa na makundi ya Watu waovu, Wasio na Imani ya Dini wala Ubinaadamu, wanaopata kinga ya kulindwa na ufadhili wa Idara za Kijasusi za Mataifa na dola za Magharibi kwa lengo lao ovu la kutaka kuupaka Matope Uislamu na Waislamu duniani.
Samahat Sheikh.Hemed Jalala.




 “Kuheshimu Imani, Mila, Tamaduni na Matukufu ya Imani za Dini tofauti tofauti ni kanuni ya Msingi ya Umoja wa Kimataifa, tunawataka wakuu wa Dola za Magharibi na Amerika kuwa Vinara kuziheshimu na kutekeleza kwa vitendo kanuni na Haki hizi”alisisitiza Jalala. 

Alisema kuwa Maamuzi yasio ya Upendeleo wa kiimani na yenye Maslahi sawa kwa raia wa Imani tofauti tofauti wa Mataifa yao. Kwani ni kwa Maamuzi wanayoyafanya yenye upendeleo wa Makusudi kwa Upande mmoja wa Imani ya Dini na kukandamiza upande mwingine ndio chanzo cha kuzuka makundi yenye misimamo mikali na yenye mikakati ya kulipiza kisasi na kufanya vitendo vya Kigaidi. 

“Wanatumia gharama kubwa kukandamiza maandamano ya Amani yanayoitishwa katika nchi zao kulaani Vitendo viovu na vya kigaidi vinavyofanywa na Taifa ghasibu la Israel? Sambamba na hili tunaungana na Ulimwengu mzima kupinga Vitendo vyovyote vya kigaidi vinavyofanyika duniani kote dhidi ya Nchi na au binaadamu yeyote asiye na hatia”alisema Jalala.

Jalala aliongeza kuwa Hakuna uhuru usio na Mipaka, Matumizi mabaya ya Vyombo vya habari na Mawasiliano, Imani na Misimamo inayokiuka mipaka ya Dini na Sheria za Nchi, Mauaji na Udhalilishaji wa Viongozi wenye kuheshimiwa wa Dini na Nchi, Kukashifu na Kutakana Matukufu ya Dini na uvunjaji wa Alama za dini zinazoheshiwa na waumini wa Dini hizo, ni Vitendo Viovu.

No comments: